Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Juma Zuberi Homera akikagua Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera Januari 05, 2021 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
IOI
Akiwa Nsimbo Komredi Homera amekagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unaoendelea katika eneo la Isinde lililoko Mji Mdogo wa Nsimbo ambapo ameridhishwa na hatua ulikofikia ujenzi wa majengo ya Hospitali hiyo. Pia ameridhishwa na kasi ya ujenzi unaozingatia viwango, ubora pamoja na matumizi sahihi ya Fedha za umma.
Komredi Homera pia amekagua Ujenzi wa Jengo la Utawala linaloendelea kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo amemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa anazingatia ubora pamoja na muda wa kukamilika kwa Ujenzi huo kwa wakati ili Wataalamu wa Halmashauri waweze kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi.
Aidha Komredi Homera amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani pamoja na Wataalamu wote kwa namna wanavyoshirikiana kusimamia vema Miradi ya Maendeleo.
Ametoa rai kwa Wananchi wa Nsimbo kujiandaa kupata huduma bora za Afya muda mfupi ujao pindi ujenzi utakapokamilika.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa