Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Juma Zuberi Homera( Mbele katikati) akiwa katika ukaguzi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Nsimbo ulioko katika hatua za mwisho kukamilika katika eneo la Isinde Kata ya Mtapenda Mji mdogo Nsimbo .Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani
Na: John .A. Mganga
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wametakiwa kujiandaa kuanza kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya inayoendelea kujengwa ambayo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho na za kuridhisha.
Katika Ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera Januari 05, 2021 aliyoifanya kwa lengo la kukagua hatua ulikofikia Ujenzi wa Hospitali hiyo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa hatua ulikofikia Ujenzi wa miundombinu ya Hospitali hiyo ambapo amewataka Wananchi kujiandaa kuhudumiwa na Hospitali hiyo.
Usimamizi makini wa Mradi chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani pamoja na Wataalamu wengine wanaohusika katika usimamizi wa mradi huo,Ujenzi unaozingatia ubora na viwango, nidhamu pamoja na na matumizi sahihi ya Fedha za Serikali ni miongoni mwa mambo yaliyomfurahisha zaidi Mh.Homera katika Ziara yake hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani katika taarifa yake, amemuambia Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Juma Zuberi Homera kuwa, Halmashauri imepokea Kiasi cha Shilingi Mil.500 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo mpaka sasa Ujenzi uko katika hatua za Mwisho kukamilika.
Mkurugenzi Mohamed amesema Ujenzi wa Miundombinu ya Majengo ya Hospitali hiyo ya Wilaya uliathiriwa na changamoto ya Msimu wa Masika jambo lililopelekea kupungua kwa kasi ya Ujenzi lakini hata hivyo ujenzi huo umeendelea na uko katika hatua nzuri na za kuridhisha.
Akizungumzia kuhusu matumizi ya Fedha Mkurugenzi Mohamed amesema mpaka sasa Kiasi ha Shilingi Milioni Mia Nne Hamsini na Saba,Laki tano sabini na nane Elfu Mia moja arobaini na tatu ( 457,578,143) kimetumika katika Ujenzi huo kati ya Milioni 500 zilizopokelewa kutoka Serikali kuu,ambapo kiasi cha Shilingi Milioni Thelathini na nne Laki nane Hamsini na tatu Elfu na Shilingi mia moja thelathini na sita(34,853,136) zilizobaki zinatarajia kupelekwa kwa jili ya Ununuzi wa Madirisha ya Alluminium.
Aidha Mkurugenzi Mohamed amesema mpaka sasa kwa upande wa Malighafi tayari Halmashauri imekwisha nunua zaidi ya Mifuko Mia sita 600 ya Saruji kwa ajili ya kuwekea Marumaru, kwa majengo yote matatu,Marumaru zote zimekwisha fika,Uwekaji wa kiambo umeme ambapo kazi iliyobakia ni kuweka Skiming,rangi pamoja na Marumaru.
Mkurugenzi Mohamed amewahakikishia Wananchi wa Nsimbo kuwa Ujenzi wa Hospitali hiyo utakamilika ndani ya muda mfupi ujao na punde Wananchi wataepuka changamoto ya kutembea umbali mrefu zaidi ya Kilomita 16 kwenda kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : +2552955164
Simu: +255713992124
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa