Pichani:Mkuu wa Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji Bi.Victoria Cilewa akiwasilisha mbele ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi(Hawako pichani) Rasimu ya Bajeti ya Mwaka mpya wa Fedha 2022/2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Na: John Mganga-DIO
Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo limepitisha makadirio ya Bajeti ya Halmashauri ya Shilingi 20,095,372850.00 kwa Mwaka ujao wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kutekeleza programu mbalimbali zilizopangwa katika ngazi ya Halmashauri.
Mkuu wa Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Victoria Cilewa Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa Mwaka mpya wa Fedha 2022/2023 amewaambia Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri kuwa makadirio hayo ni sawa na ongezeko la Asilimia 0.98 yakilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 ambayo ilikuwa Shilingi 20,668,252,869.00
Ameeleza kuwa kati ya kiasi hicho cha Fedha,Shilingi 10,106,187,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara,Shilingi 2,071,685,000.00 ni kwa ajili ya matumzi mengineyo ambapo Shilingi 7,917,500,850,00 imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Katika rasimu hiyo ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 imeelezwa kuwa Halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi 1,327,189,000.00 ambapo Shilingi 1,021,980,000.00 ni vyanzo visivyolindwa(Ownsource Proper) na Shilingi 305,209,000.00 ni kutokana na vyanzo lindwa.-Bima ya Afya,NHIF,Mfuko wa Afya ya Jamii CHF pamoja na User Fee.
Aidha katika Bajeti hiyo ya Shilingi 1,021,980,000.00 cha mapato ya ndani kilichoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Asilimia 40 sawa na Shilingi 408,792,000.00 itatumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo Shilingi 613,188,000.00 sawa na Asilimia 60 imegawanya kwenye Idara kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Wajumbe wa Baraza la Wafanya kazi wote kwa pamoja wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kufanikisha maandalizi ya rasimu hiyo ya Bajeti.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Picha 1:Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichoketi kujadili Rasimu ya Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Picha 2:Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambae ni muwakilishi wa Vijana kutoka Chama cha Walimu Tanzania CWT Nsimbo Mwalimu Felix Ferdinand akitoa mchango wake wakati wa kujadili Rasimu ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Picha 3;Shukuru Mukaruka Mjumbe wa Baraza la Wafnyakazi ambae ni Mjumbe wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa akichangia mada baada ya Rasimu kuasilishwa.
Picha 4;Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakisikiliza Rasimu ya Bajeti ya Mwaka Ujao wa Fedha 2022/2023 ilipowasilishwa na Afisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa