Vyama vya Ushririka vya Ufugaji Nyuki katika Halmashauri za Wilaya ya Tanganyika na Nsimbo Mkoani Katavi leo vimekabidhiwa vituo vya kukusanyia mazao ya Nyuki katika Hamashauri hizo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Mrindoko, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Onesmo Buswelu amehimiza wananchi na wadau wote kuendelea kutimiza wajibu wa kutunza mazingira ili kuepukana na changamoto zinazojitokeza katika ufugaji wa nyuki.
Mheshimiwa Buswelu amesisitiza wadau na watendaji wa chama cha ushirika cha ufugaji Nyuki katika Halmashauri hizo kuzitumia na kutunza vitendea kazi Pamoja na rasilimali zote walizokabidhiwa ili viweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu kwa maendeleo ya vyama hivyo katika Halmashauri zao. “Ni jukumu langu kuwahimiza kusimamia kikamilifu uendeshaji wa vituo hivi ili vipate kudumu kwa muda mrefu, vikatekeleze mpango wa kibiashara, mpango wa kiuchumi, mpango wa kimkakakti wa kumkwamua mtanzania…………..” Ameongeza Mheshimwa Buswelu
Mkuu huyo wa Wilaya ya Tanganyika amesisitiza kuwa ni lazima kila mwanachama kuwajibika katika kuongeza mnyororo wa kuongeza thamani ya mazao ya nyuki hasa asali ili kuboresha mazao hayo na hatimaye kupata soko la uhakika katika masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, Mheshimwa Buswelu amewahimiza watendaji wote wa BEVAC pamoja na viongozi wengine kushirikiana katika utafutaji wa masoko ya mazao ya nyuki kwa namna tofauti pamoja na matangazo mbalimbali na mitandao ya kijamii ili mazao yatakayokusanywa yapate masoko ndani na nje ya nchi. “Simamieni, shirikianeni kutafuta masoko, tusije tukakusanya asali hapa tukakosa masoko, dunia sasa hivi imebadilika, tumieni kila aina ya matangazo kama mitandao ya kijamii, mikusanyiko mbalimbali kufikisha taarifa zenu za mazao ambayo mtakusanya hapa……….” Ameongeza DC Buswelu
Mheshimiwa Onesmo Buswelu amewahimiza Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya za Tanganyika na Nsimbo pamoja na Maafisa kutoka vitengo tofauti kuendelea kuwapa mafunzo na semina zitakazowasaidia watendaji wa BEVAC kuendelea kuimarika katika uzalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki.
Awali akitoa taarifa ya Mradi huo, Meneja wa BEVAC Nchini Tanzania Bwana Stephen Paul amesema katika Mkoa wa Katavi, Mradi wa BEVAC unatekelezwa katika Halmashauri ya Nsimbo, Tanganyika na Mlele ambapo unatekeleza miradi mbalimbali ikiwepo kuanzisha hifadhi za nyuki kwenye misitu katika vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na Nsimbo, kuanzishwa kwa Mashamnba darasa katika Halmashauri ili kurahisisha mafunzi kwa vitendo kwa watendaji wa BEVAC.
Bwana Stephen amesema kuwa BEVAC imefanikiwa kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali kama mafunzi cherehani, seremala na kuwaunganisha wafugaji wa nyuki ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa