Taasisi ya Enabel kupitia mradi wa kuongeza mnyonyoro wa thamani wa ufugaji nyuki yaani Beekeeping Value Chain Support (BEVAC) limekabidhi Vifaa mbalimbali vya TEHAMA kwa Chama cha Ushirika cha Ufugaji Nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi.
Akikabidhi Vifaa hivyo vya TEHAMA leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini kwa Mwenyekiti wa Chama hicho cha Ushirika cha ufugaji Nyuki wilayani Nsimbo Bwana Said Mkopi pamoja na wajumbe wengine, Bi. Christina Bunini amewataka wanachama hao kuvitumia vifaa hivyo kwa usahihi na kuvitunza katika hali ya usalama wakati wote ili viweze kuwasaidia katika majukumu yao ya kila siku na kuboresha huduma zao kwa jamii.
Bi. Bunini ametumia wasaa huo kuwapongeza wanachama wote kwa kazi nzuri inayofanywa na wanachama kupitia mradi wa BEVAC na kuwatakia majukumu mema watendaji wote wa chama hicho hasa jukumu la kuboresha shughuli za chama hicho cha Ushirika cha Ufugaji Nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Aidha, kwaniaba ya wanachama wote, mwenyekiti wa chama hicho cha Ushirika cha Ufugaji Nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bwana Said Mkopi amewashukuru wadau wote na kuhaidi ushirikiano mkubwa hasa katika shighuli za kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki.
Kwa upande wake, Afisa Nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bwana Said Mpumbi amesema Vifaa hivyo vya TEHAMA vitawasaidia kuboresha utendaji kazi wa wanachama katika mazingira yao ya kazi, jambo litakalorahisisha utatuzi wa changamoto zitakazojitokeza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni Pamoja na Printa 1, Kompyuta (Desktop) 1 pamoja na Vipima unyevu ( reflactometer) 2. Vifaa vingine vilipokelewa na Chama hicho ni Pamoja Ndoo za lita 20 zipatazo 100, bomba za moshi (bee smoker) 10, brashi za nyuki (bee brush) 30 na bango 1.
Pichani ni Wanachama wa chama cha Ushirika cha ufugaji Nyuki wakipokea Vifaa vya TEHAMA kutoka Taasisi ya Enabel kupitia mradi wa kuongeza mnyonyoro wa thamani wa ufugaji nyuki yaani Beekeeping Value Chain Support (BEVAC)
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa