Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel Bunini amewaalika wananchi wote kuhudhuria ili kushuhudia matukio mbalimbali yatakayofanyika katika mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani utakaofanyika siku ya Jumanne ya Disemba 2, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo kuanzia saa 06:30 mchana.
Itakumbukwa kuwa Oktoba 29, 2025, kulifanyika uchaguzi mkuu nchini, ambapo Watanzania wenye sifa walitumia haki yao ya kikatiba kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Katika mkutano huo wa kwanza, jumla ya madiwani 12 kutoka katika Kata tisa kati ya hao madiwani watatu (03) wakiwa wa viti maalum watakula kiapo, ili kuanza kuwatumikia wananchi wao.
Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na Madiwani wateule kula kiapo, uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri, uundwaji wa Kamati za kudumu za Halmashauri, kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kuanzia Julai 2025 hadi Novemba 2025 pamoja na kupitisha ratiba za vikao vya Halmashauri.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa