Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo iko katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi wa soko jipya pamoja na stendi ya kisasa katika kitongoji cha Magula kilichopo kata ya Stalike, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi. Hayo yamebainishwa na Kaimu afisa mipango na uratibu bwana Yohana Edward Malimi alipokuwa kwenye kikao kidogo cha hadhara pamoja na wananchi wa kitongoji hicho Januari 22, 2026.
Bwana Malimi amesema kuwa, lengo kuu la kikao hicho ni kuzungumza na wananchi wa Magula pamoja na kutathimini hali ya uhitaji wa huduma hizo kwa wananchi hao ambapo kikao hiko kimeenda sambamba na zoezi la kuchukua sahihi za maridhio ya ujenzi wa miradi hiyo, na kubainisha kuwa mwitikio wa wananchi katika zoezi hilo umekuwa ni mkubwa hali inayoashiria utayari wao wa kupokea ujenzi wa miradi hiyo ya mandeleo ndani ya kijiji hiko.
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Mtisi ameishukuru serikali kwa kuwekeza ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo katika kijiji hiko na kuomba ujenzi uanze na kukamilika mapema ili kuondoa kero za muda mrefu walizokuwa wakipata wananchi wa eneo hilo kutokana na kutokuwa na Soko pamoja na stendi rasmi ya magari katika eneo hilo.
Ujenzi wa Soko na Stendi Mpya katika eneo hilo unatarajia kuwa mkombozi wa huduma hizo kwa Wananchi wa maeneo hayo kwani wamekuwa wakipata huduma hizo katika Soko na Stendi ndogo iliopo katika eneo hilo huduma ambazo zimekuwa hazikidhi uhitaji wa wananchi kutokana na ongezeko kubwa la watu katika maeneo hayo.


Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa