Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amemteua Mheshimwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akisoma uteuzi huo wa Mheshimiwa Rais mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma mapema hii leo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu amesema: “Kwa kutekeleza matakwa hayo ya kikatiba, nimemteua mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania…….” Imesema sehemu ya ujumbe huo.
Baada ya kutangazwa uteuzi huo na baadaye kuthibitishwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema anautambua vizuri umasikini uliopo nchini.
"Mimi umasikini wa Tanzania sijausoma kwenye kitabu nimeuishi, miaka takribani 32 nimeishi katika maisha hayo ya umasikini", …… "Unaenda kuchunga ukirudi nyumba nzima inavuja, natambua maisha haya". alisema Mheshimiwa Dkt. Nchemba mara baada ya kuthibitishwa Bungeni.
Itakumbukwa kwamba, mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, 29 mwaka huu.
Tangu baada ya Uhuru wa Tanganyika na baadaye Tanzania (1961), Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba anakuwa Waziri Mkuu wa kumi na mbili (12) akipokea kijiti kutoka kwa Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa aliyehudumu katika nafasi hiyo tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwezi Novemba 2015.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa