Pichani:Kaimu Mkurugenzzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa akizungumza na Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Ugalla alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo hicho 22 Machi 2022.
Nsimbo-Ugalla
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa leo 22 Machi 2022 akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoko katika Kata ya Ugalla Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Akiwa Ugalla Bi Tabia amekagua maendeleo ya Ujenzi wa kituo cha Afya Ugalla kinachojengwa ambapo amejiridhisha kuendelea kwa shughuli mbalimbali za ujenzi bia kuwepo kwa changamoto zozote katika eneo la Ujenzi wa Kituo hicho cha Afya.
Bi Tabia amewapongeza mafundi kwa namna wanavyojitoa mpaka hatua ulipofikia ujenzi huo ikiwa ni tangu alipotembelea ujenzi huo 17 Machi 2022 akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Bi Jamila Yusuph Kimaro.
Kaimu Mkurugenzi Tabia amewasisitiza kamati ya Ujenzi pamoja na Wasimamizi wengine wa mradi huo kuhakkiisha kuwa wanafanya manunuzi ya vifaa kwa wakati badala ya kusubiri Vifaa viishe ndipo waanze mchakato wa manunuzi kwa kuwa kufanya hivyo ni kuathiri utekelezaji wa mradi jambo linaloweza kusababisha mradi kutokamilika kwa wakati.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Nsimbo amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Maabara katika Sekondari ya Ugalla ambapo amejiridhisha kwa maendeleo mazuri ya Ujenzi wa mradi huo ambao kwa sasa upo katika hatua za Umaliziaji.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa