Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kutambua umuhimu wa zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 23, Agosti 2022 ambapo watu wote watakao lala ndani ya mipaka ya nchi usiku wa kuamkia siku ya Sensa watahesabiwa (Raia wa Tanzania na Asiye Raia), Halmashauri imeendelea na maandalizi ya kuhakikisha lengo hilo linafikiwa kwa asilimia mia na kwa ufanisi mkubwa.
Mratibu wa Sensa ya watu na Makazi ndugu Scholastika Njovu kwa kushirikiana na kamati ya Sensa ya watu na makazi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wameendelea kutoa elimu ya Sensa ya watu na makazi kwa kamati za Sensa ya watu na makazi ngazi ya Vitongoji, Vijiji, na Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Mratibu wa Sensa ameeleza elimu wanayotoa inalenga kuwajengea uwezo kamati za Sensa ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata, kwanza kutambua majukumu yao katika kufanikisha zoezi hili, pili wawe na uelewa mkubwa kuhusiana na Sensa ya watu na makazi maana wao ndio wataenda kutoa elimu na kuhamasisha jamii na kuhakikisha wananchi wanaowazunguka na kushiirikiana nao wanakuwa na uelewa wa Sensa kabla ya siku ya Sensa.
Kila mwananchi anawajibu wa kuhakikisha anahesabiwa mara moja tu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa karani wa Sensa. Ili kufanikisha hayo wananchi wanatakiwa wahakikishe wanakuwepo kwenye kaya zao siku ya zoezi la sensa ama kuacha taarifa muhimu kama Taarifa za kidemografia (Umri, Jinsi, Hali ya ndoa), Taarifa za ulemavu (Aina ya ulemavu na chanzo cha ulemavu), Taarifa za uhamiaji, Taarifa za vitambulisho vya utaifa na uhai wa wazazi, Taarifa za Elimu, Taarifa za shughuli za kiuchumi, Taarifa za umiliki wa Ardhi na Tehama, Taarifa za hali ya uzazi, Taarifa za vifo na vifo vitokanavyo na uzazi, Taarifa za nyumba, hali ya umiliki wa nyumba, vifaa/Rasilimali na udhibiti wa mazingira, Taarifa za Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Taarifa kuhusu mpango wa TASAF, Taarifa za majengo/nyumba, Anwani za makazi na Taarifa za huduma za jamii katika ngazi ya kitongoji na Mtaa.
SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa