Mfano wa Kitalu nyumba kinachoendelea kuandaliwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ili kutoa fursa kwa Wakulima wa Matunda na mbogamboga Nsimbo kujifunza katika Kituo cha Elimu ya Kilimo Nsimbo.
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (ASDPII) kwa kushirikiana na Shirika la HELVETAS Tanzania kupitia Mradi wake wa KIBOWAVI unaojihusisha na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda imeanza Ujenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kitakachotoa Elimu kuhusu mbinu bora na za kisasa za Kilimo cha Mbogamboga na matunda.
Kaimu Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Lodrick Ntulo amesema Uwepo wa Kituo hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo utasaidia kwa kiasi kikubwa Wakulima wa Nsimbo na Wilaya ya Mpanda kwa ujumla kuondokana na Kilimo cha Mazoea kisicho na Tija na kwamba kupitia Elimu itakayotolewa kituoni hapo itasaidia kuongeza Uzalishaji wa Mazao ya Matunda na Mbogamboga kwa wakulima wa Nsimbo.
Bw.Ntulo ameeleza kuwa Ujenzi wa Kituo hicho unaendelea katika Eneo la Isinde ilipo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika lango la kuingilia Halmashauri kilipo kibao kinachoelekeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilipo.
Ameeleza kuwa maandalizi ya Kituo hicho yapo katika hatua nzuri kwakuwa mpaka sasa Maji yamekwishapatikana katika Eneo hilo,na eneo kwa ajili ya Vitalu Nyumba limekwishafanyiwa Usafi,Vifaa vya umwagiliaji kwa njia ya Matone vimekwish nunuliwa na kwamba kinachosubiriwa ni Mzabuni alieshinda zabuni ya kufunga Kitalunyumba akamilishe kazi ya Ufungaji kusudi kituo kizinduliwa na kufanya kazi.
Mradi wa KIBOWAVI unatekelezwa katika Kata sita za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo katika Kata tano kutakuwepo Mashamba ya Mfano kwa ajili ya kutoa Elimu kwa wakulima katika maeneo yao juu ya mbinu bora na za Kisasa za Kilimo cha Mbogamboga na matunda.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa