• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

MADAKTARI WA SAMIA - TUMAINI JIPYA LA AFYA KWA WANANCHI WA NSIMBO

Imewekwa: September 30th, 2025

Timu Ya Madaktari wabobevu, maarufu kama madaktari wa Samia imeanza kutoa huduma za kidaktari bingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi huku idadi kubwa ya wananchi wakijitokeza kufuata huduma hizo.

Timu hiyo ya Madaktari sita (6) iliwasili hospitali hapo siku ya Jumatatu, Septemba 29, 2025, na inatarajiwa kuendesha huduma hiyo mpaka Oktoba 3, 2025.

Wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo wakiwemo Wanawake, Wanaume, Vijana pamoja na watoto walioambatana na wazazi wao, wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Madaktari hao wametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu mkubwa alioufanya kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia Wananchi katika maeneo yao na kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu ambazo wengi zilikuwa zikiwashinda kutokana na changamoto za kutomudu gharama.

“Kwa kweli tunashukuru wananchi wengi wa Nsimbo wamejitokeza kuja kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya Afya ya kinywa na meno, wengi walishajikatia tamaa lakini ujio wetu umerudisha matumaini yao. Hivyo pongezi nyingi kwa Rais Samia kuhakikisha tunakuja hapa na kuonana na Wananchi wenye shida mbalimbali. Tumewahudumia na wanaonesha matumaini ya kupona.” Amesema Dokta William Sienga, Daktari Bingwa wa afya ya Kinywa na meno kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili

“Mheshimiwa Rais ameonesha moyo wa upendo kwa kusogeza huduma za afya karibu kabisa na Wananchi wa Mkoa na Wilaya za Katavi.Tuko tayari kutoa huduma kwa Wananchi wa hapa, na mwitikio ni mzuri wengi wanakuja kupata huduma kwani vinginevyo ingewapasa wasafiri kwenda Muhimbili , Mbeya au Bugando. Hawana tena haja, huduma ziko nje ya milango yao” Amesema Hamis Paulo Mpigahodi ambae ni Daktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji kutokea Shinyanga.

“Ningewasihi Wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi, hatuombi waugue lakini kwa wale ambao wanaugua watumie nafasi hii kuja hapa kupata mustakabali wa afya zao kwani huduma tunazotoa ni za kiwango cha juu kabisa” ameendelea kusisitiza Dkota Hamis

Mbali na Madaktari, Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo waliofika hospitali hapo kupata matibabu walipata wasaa wa kuelezea furaha yao kutokana na uwepo wa kambi ya Madaktari wabobevu katika Halmashauri yao.

“Nilisikia tangazo kuhusu ujio wa Madaktari bingwa katika Halmashauri yetu ya Nsimbo, hivyo nimekuja na nimeonana na madaktari na nimepata tiba.Tunamshukuru Mungu huduma ni nzuri, tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutukumbuka wana Katavi. Napaenda kuwashauri Wananchi wenzangu wenye changamoto mbalimbali wafike hapa hospitali kwani madaktari wapo.Mwisho ningependa kumshukuru Mama Samia kwa kutukumbuka “ amesema Eunice katona kutokea Mtapenda

Vilevile Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nsimba, Dokta Patrick Tullyanje, ameonesha furaha yake kwa kuwapokea Madaktari hao bingwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.

“Tumepokea madaktari bingwa ambao wametusogezea huduma maana tulikuwa tunapata changamoto nyingi sana za Wananchi kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma, walikuwa wanasafiri zaidi ya kilomita 300 kwenda kufata huduma za kibingwa. Shukrani kwa Mheshimiwa Rais Samia kwa kuliona hilo na kutuletea hawa madaktari bingwa ambao watakaa hapa kwa wiki nzima.”

“Nitoe wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuja kupata ufumbuzi wa changamoto zao za kiafya ili tujenge taifa ambalo lina nguvu kazi yenye afya imara”

Zoezi hilo katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo limeanza Septemba 29, 2025 na litafikia tamati Oktoba 3, 2025.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA November 13, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA MRADI WA KITUO CHA AFYA IBINDI August 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MPANDA AHIMIZA UPANDAJI MITI, ASISITIZA AMANI NCHINI

    November 26, 2025
  • RC MRINDOKO AWATAHADHARISHA MAWAKALA NA WAFANYABIASHARA WA PEMBEJEO ZA KILIMO

    November 19, 2025
  • PONGEZI KWA PROF RIZIKI SHEMDOE

    November 17, 2025
  • DED NSIMBO AWATAKIA MTIHANI MWEMA WATAHINIWA WA CSEE-2025

    November 17, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa