Pichani:Wananchi katika Kata ya Kanoge wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kupata chanjo ya UVIKO 19 wakati Mtaalamu wa Afya kutoka Kituo cha Afya Kanoge akiendelea kuwapatia Chanjo.
Idadi kubwa ya Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 wakati wa Uzinduzi wa Mpango harakishi na shirikishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 uliofanyika katika Kata ya Kanoge katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Kanoge Tarehe 03 Septemba 2021.
Muitikio huo mkubwa wa Wananchi kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 ni matokeo ya nguvu kubwa kutoka kwa Wataalalmu wa Afya Nsimbo (CHMT) iliyoelekezwa katika kutoa Elimu na Hamasa kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kupata Chanjo ya UVIKO 19.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mpango Harakishi na Shirikishi wa utoaji wa Chanjo ya UVIKO 19 Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kanoge Bw.Salehe Msompola amewaambia Wananchi wa Kata ya Kanoge kuwa ni muhimu kupata chanjo ya ya UVIKO 19 ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza endapo mtu hatapata chanjo ya hiyo.
Makamu Mwenyekiti huyo amewataka Wananchi kupuuza uzushi unaoenezwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao kisiasa kuwa chanjo hiyo si salama kwa matumizi ya binadamu na kwamba ni njama za Wazungu kuwaangamiza Waafrika Duniani na badala yake Wananchi kujikita zaidi kusikiliza maelekezo ya Wataalalmu wa Afya Nchini.
Msompola ameongeza kuwa endapoio Jamii ya Kitanzania itahamasika kupata chanjo ya UVIKO 19 itasaifia kwa kiasi ikubwa kupunguza na kuondoa kabisa Ugonjwa wa UVIKO 19 na kwamba Taifa litarejea katika hali ya kawaida na Wananci watapiga hatua kimaendeleo huku akiataka waliokwisha chanja UVIKO 19 kuwa mabalozi kuwahamasisha wengine ili waweze kupata chanjo hiyo.
Akiwasilisha Taarifa ya hali ya Utoaji wa chanjo ya UVIKO19 katika Halmashaurii ya Wilaya ya Nsimbo,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Ismail Kanani amesema Halmashauri imepokea dozi 1700 kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya makundi maalumu na makundi ya kipaumbele na kufuatiwa na watu wenye umri kuanzia miaka 18.
Ameyataja makundi ya kipaumbele kuwa ni Watumishi wa Afya,Skta ya Utalii,Walimu pamoja kundi la watu wanaosumbuliwa na magonjwa Sugu ikiwemo Sukari,Magonjwa ya Moyo nk.
Mganga Mkuu Kanani ameeleza kuwa mara baada ya kupokea dozi hizo za chanjo Halmashauri ilizindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo kwa makundi maalumu katika kituo cha Afya Katumba ambapo vituo vingine viwili ambavyo ni kituo cha Afya Kanoge na Kituo cha Afya Mtisi viliandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma za chanjo ya UVIKO 19.
Ameeleza kuwa hadi sasa huduma ya chanjo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inaendelea kutolewa katika vituo 21 vya kutolea huduma za afya ambapo watu 946 kati yao Wanaume 554 na wanawake 392wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19 ambapo mpaka hivi sasa hakuna kisa chochote kuhusu madhara makubwa ya chanjonya UVIKO 19, isipokuwa maudhi madogomadogo yanayotokea kaa ilivyo katika matumizi ya dawa nyinginez za binadamu.
Mpango harakishi na shirikishi wa utoaji wa Chanjo ya UVIKO 19 unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo kampeni na Hamasa vinaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata chanjo ya UVIKO 19.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa