Pichani:Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo na Diwani wa Kata ya Ugalla Mh.Halawa Charles Malendeja akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bulembo waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa Mnada wa Mifugo Bulembo 13 Septemb 2021.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Halawa Charles Malendeja ametoa rai kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kutumia fursa ya Minada inayoanzishwa kufanya biashara ili kujikwamua na umasikini
Mwenyekiti Malendeja ameyasema hayo alipotembelea mnada mpya ulioanzishwa katika Kijiji cha Bulembo Septemba 13 2021 ikiwa ni jitihada za Halmashauri kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kupitia minada mbalimbali ndani ya Halmashauri.
Amesema kuanzishwa mnada wa Bulembo ni Fursa kwa Wananchi wa Kata ya Bulembo kupanua wigo wa baiashara jambo litakaloinua kipato cha mtu mmojammoja na hatimae maendeleo katika Kata ya Litapunga yataonekana na kwamba umasikini utatoweka
Afisa Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Daniel Walakunga amesema mnada ulioanzishwa katika Kijiji cha Bulembo Litapunga utakuwa ukifanyika kila Siku ya Jumatano kufuatia maoni mbalimbali yaliyotolewa na Wafanyabiashara katika Mnada huo mpya wa Bulembo.
Amesema Halmashauri itaendelea kuanzisha minada kila itakapohitajika lengo likiwa ni kupanua wigo wa Biashara ambapo mpaka sasa minada mbalimbali ya Mifugo imeanzishwa ndani ya Halmashauri ili kuhakikisha kuwa Ushuru wa Mifugo unatozwa ipasanyo.
Walakunga ameongeza kuwa kuansishwa kwa Mnada huo ni jitihada za Halmashauri kupanua wigo wa ukusanyaji mapato kupitia tozo za ushuru wa bidhaa mbalimbali zitakazokuwa zikiuzwa ndani ya mnada huo hususani Ushuru wa Mifugo
Amesema Lengo ni kufanya mnada wa Bulembo kuwa mnada mkubwa wa Mifugo jambo litakalosaidia Halmashauri kukusanya kwa urahisi Ushuru wa Mifugo na pia kusaidia kwa sehemu kubwa kuboresha mazingira ya Wafugaji kufanya biashara na kujipatia kipato na kwamba kabla ya kuanza kutoza ushuru watajenga mazingira rafiki yatakayowezesha mnada huo kukua
Wafanyabiashara walioshiriki katika mnada huo mpya wa Bulembo wameiomba Halmashauri kujenga mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na miundombinu ya Vyoo sambamba na kuvuta subira ili biashara ishamiri kabla ya kuanza kutoza ushuru jambo ambalo linaweza kuathiri kwa haraka kukua kwa mnada huo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa