Katika jitihada za kuinua uzalishaji wa zao la Karanga kwa wakulima, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inatarajia kusambaza Mbegu bora ya zao la karanga kwa wakulima wa zao hilo ili kuinua uzalishaji na kufanya Kilimo cha zao hilo kuwa chenye tija zaidi.
Kaimu Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Lodrick Ntulo amesema Halmashauri imepokea Mbegu ya Karanga kiasi cha Kilo 100 aina ya Naliendele 16 zilizopokelewa Tarehe 27 Septemba 2021 kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania kituo cha Naliendele.
Aidha Taasisi hiyo pia imetoa Kilo mbili za Mbegu ya Karanga aina ya Mnanje na Nachingwea kwa kila Kata kwa Kata 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa ajili ya mashamba Darasa ya Kata hizo kwa ajili ya Wananchi kujionea na kujifunza ubora wa mbegu hizo.
Akizungumzia kuhusu kilo 100 za Mbegu mpya ya Naliendele 16 Bw.Ntulo amesema Halmashauri kupitia Idara ya Kilimo na Ushirika itasambaza mbegu hizo kwa wakulima wa zao la Karanga watakaoteuliwa na Maafisa Ugani kutoka Kata zote 12 za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo wakulima hao watagawiwa mbegu hizo kusudi waweze kuotesha na baadae kuzisambaza kwa wakulima wengi zaidi.
Uzalishaji wa zao la Karanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika msimu wa kilimo uliopita wa mwaka 2019/2020 ulishuka kutokana na changamoto ya Ugonjwa wa Mnyauko Fuzali ambao ulisababisha kupungua kwa mavuno.
Kutokana na changamoto hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilifanya mawasiliano na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Kituo cha Naliendele kwa ajili ya kutafuta suluhu ya changamoto ya Ugonjwa wa Mnyauko Fuzali ulioathiri uzalishaji wa zao la Karanga katika Msimu wa Kilimo wa mwaka 2019/2020.
Taasisi hiyo ilileta aina sita za Mbegu ya zao la Karanga zenye uwezo wa kuhimili Ugonjwa wa Mnyauko Fuzali na kuzigawa kwa wakulima ambapo baada ya wakulima kuifanyia majaribio waliipeda Mbegu ya zao la Karanga aina ya Naliendele 16 ambayo ilifanya vizuri katika msimu wa kilimo 2020/2021.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa