Halmashauriya Wilaya ya Nsimbo imeonyesha dhamira ya dhati ya kukuza mapato yake kupitiachanzo cha madini, hatua inayolenga kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboreshamaisha ya wananchi wa Halmashauri hiyo. Dhamira hii ilidhihirika kupitia ziaraya madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo, wakiambatana na Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri hiyo, Eng. Stephano B. Kaliwa, pamoja na baadhi ya wataalamu naviongozi wa chama tawala. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuongeza ujuzi nauzoefu katika mbinu bora za ukusanyaji wa mapato, hususan kupitia rasilimali zamadini.
Walipokelewakwa ukarimu na wenyeji wa Halmashauri ya Nyang’wale na Geita, ambapo walifanyakikao kifupi cha mafunzo. Katika kikao hicho, wenyeji walieleza namnawanavyokusanya mapato kwa kutumia vyanzo vya madini, na kuwaonyesha mifanohalisi kwa kuwapitisha kwenye maeneo ya migodi. Madiwani na viongozi wa Nsimbowaligundua vyanzo vipya vya mapato ambavyo wamekusudia kuviweka kwenye sheriandogo za halmashauri yao ili kuhakikisha vyanzo hivyo vinatumika ipasavyokatika ukusanyaji wa mapato.
WalitembeleaHalmashauri ya Nyang’wale, hususan mgodi mdogo wa Isonda Gold Minersunaomilikiwa na mzawa, na Halmashauri ya Geita Mjini, ambapo walijifunza mbinumbalimbali za kubuni na kutekeleza vyanzo vya mapato. Katika ziara hiyo,walibaini umuhimu wa kutunga na kutekeleza sheria ndogo zitakazowezeshaukusanyaji wa ushuru kwa uhalali katika vyanzo vipya vya mapato, hatua ambayoinalenga kuongeza mapato ya halmashauri hiyo kutoka shilingi bilioni 1.8 hadibilioni 3 kwa mwaka.
MkurugenziMtendaji, Eng. Stephano B. Kaliwa, alisisitiza kuwa halmashauri hiyo ipo tayarikubuni mikakati thabiti na kuweka sheria ndogo zitakazowataka wachimbaji wadogowa madini kufuata taratibu za ulipaji ushuru. Sheria hizi zinalenga kuimarishauwajibikaji na kuhakikisha mapato yanayokusanywa yanatumika kwa maendeleo yajamii, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii na kuinua uchumi wa eneohilo.
Hatuahii ni muhimu sana kwa Halmashauri ya Nsimbo, kwani itahakikisha rasilimalizake za madini zinatumika kikamilifu kuchangia maendeleo ya kiuchumi nakuboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa