Pichani : Muonekano wa Jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo likiwa katika hatua za Mwisho za Umaliziaji hdi kufikia 17 Machi 2022
Ujenzi wa Jengo jipya la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo unaoendelea hivi sasa uko katika za hatua za Mwisho za Umaliziaji.
Nsimbo-Mtapenda
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Nsimbo Mhandisi Martin Kasonso amesema kwa sasa itachukua kipindi kisichozidi Mwezi mmoja kwa watumishi kuhamia katika Jengo hilo la utawala kwa kuwa kwa sasa Ujenzi huo upo katika hatua za mwisho za Umaliziaji.
17 Machi 2022 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa alitembelea eneo la mradi kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo hilo la Utawala ambapo amejiridhisha kuendelea kwa shughuli za Ujenzi katika hatua ya umaliziaji.
Ujenzi wa Jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ulianza rasmi Mwaka 2017 ambapo utekelezaji wake umechukua muda kutokana na Ujenzi huo kuendelea kwa kadiri Serikali ilivyokuwa ikitoa fedha.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa