• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

NSIMBO YAADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO KWA USAFI, UPANDAJI MITI NA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

Imewekwa: April 26th, 2025

Katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo leo Aprili 26, 2025, imefanya shughuli mbalimbali ikiwemo usafi wa mazingira, upandaji wa miti, na ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Shughuli hizo zimefanyika katika maeneo ya Ofisi ya Halmashauri, Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo, na Kata ya Itenka, zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda aliyewakilishwa na Afisa Tarafa. Watumishi wa Halmashauri, wananchi na viongozi mbalimbali wameshiriki kikamilifu katika shughuli hizo.

Katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa, miti mbalimbali imepandwa katika maeneo tofauti ndani ya Kata ya Itenka ikiwa ni sehemu ya kampeni endelevu ya kutunza mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, viongozi wamefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Sekondari Anna Lupembe iliyopo Kata ya Nsimbo, mradi unaokaribia kukamilika. Mradi huu ulianza tarehe 1 Oktoba 2024, na hadi sasa umetumia kiasi cha Shilingi 76,139,005.27 kati ya Shilingi 110,000,000 zilizotengwa, huku kiasi kilichobaki cha Shilingi 33,860,994.27 kikiendelea kusimamiwa ili kukamilisha kazi zilizobakia.

Walimu wa Shule ya Sekondari Anna Lupembe pamoja na viongozi wa Halmashauri wamemshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha nyingi zilizowezesha ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu.

Walimu hao wamesema kuwa mradi huu umekuwa suluhisho kubwa kwa changamoto ya kuishi mbali na shule, hali ambayo awali ilisababisha usumbufu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao. Waliahidi kuhamia mara moja katika nyumba hiyo baada ya kukamilika, na kutimiza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa kwa manufaa ya wanafunzi na maendeleo ya sekta ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Tarafa amewataka wananchi kuendelea kuenzi Muungano kwa vitendo kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kulinda mazingira na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.

“Muungano Wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa — Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.”


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA November 13, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA MRADI WA KITUO CHA AFYA IBINDI August 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RC MRINDOKO AWATAHADHARISHA MAWAKALA NA WAFANYABIASHARA WA PEMBEJEO ZA KILIMO

    November 19, 2025
  • PONGEZI KWA PROF RIZIKI SHEMDOE

    November 17, 2025
  • DED NSIMBO AWATAKIA MTIHANI MWEMA WATAHINIWA WA CSEE-2025

    November 17, 2025
  • HONGERA SANA DKT. MWIGULU NCHEMBA

    November 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa