Timu ya Tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo (M&E) katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeendelea kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Miradi iliyotembelewa leo na kukagauliwa ni pamoja na Ukarabati wa Soko la Sonambele iliyopo katika Kata ya Kapalala, ambapo kiasi cha shilingi milioni 20 zilipelekwa kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa vizimba katika soko hilo, ambapo hadi sasa ujenzi uko katika hatua ya umaliziaji.
Mradi mwingine ni mradi wa Ukarabati wa Zahanati ya Kajeje, ambapo kiasi cha shilingi milioni 20 zilipelekwa huko kukamilisha mradi huo, Ambapo hadi sasa mradi huo uko katika hatua ya umaliziaji. Aidha, mkandarasi anayetekeleza mradi huo amepewa muda wa wiki moja kuhakikisha kazi zilizobaki, ikiwa ni pamoja na kupiga msasa na kupaka rangi zimekamilika ndani ya wiki moja.
Aidha, Katika mradi wa Ukarabati wa vyoo katika Soko la Kanoge, timu hiyo imefanya ukaguzi wa matundu 12 ya vyoo katika soko la Kanoge ambapo ukarabati wa vyoo hivyo unatarajia kufanyika kwa haraka na mradi huo unatarajia kukamilika kabla ya tarehe 31 desemba 2025. Kiasi cha shilingi milioni 10 zimetengwa kwaajili ya mradi huo.
Timu hiyo imeendelea na ukaguzi katika mradi mwingine ambao ni mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Awali na Msingi, unaotekelezwa katika Kijiji cha Katambike Kata ya Ugalla. Katika mradi huu, kiasi cha shilingi milioni 342.9 zimepelekwa kwaajili ya mradi huu, ambapo hadi sasa ujenzi wa Jengo la Utawala na majengo yenye jumla ya Madarasa 6 ya elimu msingi unaendelea na upo katika hatua ya jamvi.
Mradi mwingine ni mradi wa umaliziaji wa nyumba ya watumishi yenye uwezo wa kutumiwa na familia mbili za watumishi yaani (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Ugalla River. Katika Mradi huu, kiasi cha shilingi milioni 40 zilipelekwa katika mradi huo ambapo hadi sasa mradi huo uko katika hatua za mwisho kukamilika ambapo mkandarasi amepewa wiki moja kukamilisha kazi ya upigaji rangi na kuweka marumaru ili mradi huu uanze kutumika.
Aidha, timu hiyo ilifika katika mradi mwingine wa Stendi ya Mabasi katika kata ya Ugalla, Timu imetembelea na kukagua eneo la mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi katika kata ya Ugalla ambapo ukaguzi umefanyika katika hatua ya awali hasa mipaka ya eneo lililotengwa kwaajili ya mradi huo.
Aidha, mradi mwingine ni mradi wa Umaliziaji wa Majengo katika Kituo cha Afya Ugalla. Ambapo katika mradi huu, Kiasi cha sh. milioni 40 zilipelekwa kwajili ya umaliziaji wa miundombinu katika jengo la Mama na Mtoto, Maabara na Jengo la wagonjwa wa nje. Hadi sasa jengo la mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji na wodi ya wanawake limekamilika.
Katika miradi yote iliyotembelewa na timu hiyo, wajumbe waliongonzwa na Bwana Julius Moshi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Bunini waliwasihi wakandarasi kuongeza kasi ili kukamilisha miradi hiyo kwa haraka na kwa viwango vinavyotakiwa na hatimaye miradi hiyo ianze kutumika na kuwasaidia wananchi.



Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa