• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

NSIMBO YAFICHUA UTAJIRI MKUBWA ULIOJIFICHA ARDHINI

Imewekwa: November 13th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi ina ukubwa wa jumla ya kilometa za mraba 14,623. Kati ya hizo, Kilometa za mraba 2,309.58 ni ardhi nzuri kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara, kilometa za mraba 8,920.03 zikiwa ni hifadhi ya misitu, kilometa za mraba 2,632.14 ni hifadhi ya wanyamapori na kilometa 292.46 ni sehemu ya maji wakati maeneo mengine yakitumika kwa shughuli zinginezo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ina jumla ya wakazi 201,102, kati yao wanaume wakiwa 100,712 na wanawake 100,390. Shughuli kubwa ya wakazi hao ni kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji wa madini na biashara.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Daniel          Bunini anafichua na kubainisha utajiri mkubwa na fursa lukuki za kiuchumi zinazopatikana katika Halmashauri hiyo. Ardhi nzuri kwaajili ya kilimo, uvuvi, uchimbaji madini, ufugaji, uwekezaji ni miongoni mwa mwa fursa lukuki zinaziiremba Nsimbo.

Kwa upande wa kilimo, Bi. Christina Bunini anaeleza kuwa Halmashauri hiyo ina hekta 230,958 za ardhi inayofaa kwa kilimo cha mazao ya chakula na biashara, ambapo ameleeza mazao makuu ya chakula yanayolimwa katika Halmashauri hiyo ni pamoja na mahindi, mpunga, mihogo, viazi vitamu, ndizi, ulezi, mboga za majani na matunda mchanganyiko. Pamoja na mazao hayo ya chakula ardhi ya Nsimbo pia ni nzuri sana kwa kilimo cha mazao ya biashara ambayo ni pamoja na tumbaku, pamba, mpunga, mahindi, karanga, alizeti, ufuta, korosho na choroko.

Uwepo wa maji ya kutosha yanayopatikana katika Halmashauri ya Nsimbo imepelekea kuboresha shughuli za kilimo jambo lililowafanya wakazi wa Halmashauri hiyo kujikita pia katika kilimo cha umwagiliaji ambapo zimeanzishwa jumla ya skimu kubwa tatu za umwagiliaji ambazo ni skimu ya Ugalla yenye jumla ya hekta 225, skimu ya Uruwira hekta 350 na skimu ya umwagigiliaji ya Usense wenye hekta 106.

Aidha, Bi. Bunini amesema wataalamu wa kilimo kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tayari wamefanya upembuzi yakinifu katika maeneo mbalimbali ili kuanzisha skimu zingine za umwagiliaji. Ameyataja maeneo ambayo yanafaa kuanzishwa kwa skimu hizo ni pamoja na Kambuzi Halt yenye jumla ya hekta 125, Ikondamoyo yenye hekta 180 na maeneo ya Kata ya Itenka yenye takribani hekta 4,500 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Shughuli za kilimo cha umwagiliaji zinafanyika katika kipindi chote cha mwaka kutokana na uwepo wa maji ya kutoka vyanzo vinavyoaminika na kuwapatia wakulima nafasi ya kuzalisha mazao ya aina mbalimbali katika kipindi chote cha mwaka.

Ili kuimarisha na kuongeza pato la kila mkulima na serikali kwa ujumla, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imejenga Ghala kubwa la kuhifadhia mazao katika Kijiji cha Uruwira inayoweza kuhifadhi jumla ya tani mia mbili (200) za mazao. Pamoja na ghala hilo, Halmashauri ya Nsimbo pia imejenga soko la mazao kilichopo katika Kijiji cha Kambuzi Halt ambalo jengo lake liko katika hatua ya umaliziaji hasa miundombinu ya kisoko kama Ofisi, vizimba, vyoo na maji safi.

Aidha, Bi. Christina Bunini anazidi kueleza kuwa shughuli za ufugaji          nazo zinazidi kushika hatamu katika kipindi hiki ambacho wafugaji wanazidi kuongezeka kutokana na uhakika wa malisho ambapo Halmashauri imetenga eneo la vitalu kumi vyenye jumla ya takribani ekari 7,752.12 kwaajili ya maeneo ya ufugaji.

Anaeleza kuwa, suala la malisho ya mifugo inaendana na uwepo wa maji hivyo Halmashauri hiyo imetumia kiasi cha shilingi milioni mia tano na kumi (Milioni 510) kwaajili ya uchimbaji wa bwawa kubwa lenye ujazo wa mita za ujazo 91,829. Uwepo wa bwawa hilo unasaidia wafugaji kutotembea na mifugo yao kufuata maji katika maeneo nje na vitalu vilivyotengwa. Wakazi wa Halmashauri ya Nsimbo wanajishughulisha na ufugaji wa ngo’mbe, mbuzi, kondoo, nguruwe, sungura, kuku, nk.

Uhakika wa uzalishaji wa mazao ya mifugo hasa maziwa umevutia baadhi ya wawekezaji, jambo linalothibitishwa na kuanzishwa kwa kiwanda cha kusindika na kuchakata maziwa cha MSS kilichopo Nsimbo.

Kwa upande wa viwanda na uwekezaji, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ina maeneo mazuri sana na yenye kuvutia wawekezaji kutokana na jiografia ya maeneo yalipo, miundombinu ya barabara zinazopitika katika kipindi chote cha mwaka, reli, umeme, maji safi na salama, afya, elimu utalii nk. Aidha, ekari zipatazo 102 zimetengwa kwa shughuli hizo za viwanda na uwekezaji.

Katika kata ya Mtapenda, jumla ya ekari 91 zimetengwa kwa ajili ya viwanda ili kurahisha huduma kwa wananchi ambapo kati ya ekari hizo, ekari 51 tayari zimepata wawekezaji.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ina eneo lingine lililopo Msaginya Kata ya Nsimbo lenye jumla ya ekari 11 kwaajili ya viwanda na uwekezaji.

Pamoja na shughuli zote hizo, ardhi ya Halmashauri ya Nsimbo pia ina utajiri mkubwa wa madini mbalimbali kama dhahabu, chuma, zinki, shaba, nk, ambapo wachimbaji wadogo wanajishughulisha na shughuli hiyo katika maeneo yanakopatikana madini hayo hasa Msaginya, Ibindi, Kapalala, Machimboni, Nsimbo Ugalla, nk.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA KIDATO CHA KWANZA 2026 December 04, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA MRADI WA KITUO CHA AFYA IBINDI August 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA November 13, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RC MRINDOKO AHIMIZA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO – NSIMBO DC

    December 17, 2025
  • KAMATI YA SIASA MPANDA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO H/W NSIMBO

    December 19, 2025
  • DC MPANDA AHIMIZA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI WA AWALI NA MSINGI

    December 10, 2025
  • NSIMBO YAJIDHATITI KUSIMAMIA VIZURI MIRADI YA MAENDELEO - WAKANDARASI WAAGIZWA KUONGEZA KASI.

    December 04, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa