Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imepokea kiasi cha shilingi Bilioni moja na Milioni kumi (1,010,000,000/=) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimabali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika kutekeleza kwa ufanisi miradi hiyo iliyolengwa na kupewa kipaumbele, fedha hizo zimegawanywa katika miradi mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu na miradi mingine hususani utawala.
Kwa upande wa Afya shilingi milioni mia mbili (200,000,000) zimetengwa kwaajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya nakatika Zahanati mbalimbali vilivyopo Halmashauri ya Nsimbo.
Aidha, kwa upande wa elimu kiasi cha shilingi milioni mia moja na kumi (110,000,000/=) zimetengwa kwaajili ya miradi ukamilishaji wa maabara katika shule za sekondari na umaliziaji wa madarasa katika shule za msingi.
Sambamba na miradi hiyo ya Elimu na Afya, jumla ya shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa majengo ya utawala pamoja na ufutiliaji na tathmini ya miradi katika Halmashauri ya Wilaya Nsimbo
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa