Afisa Mwandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Jimbo la Nsimbo ameeleza kuwa Daftari la Awali la Wapiga Kura la Awamu ya Kwanza litawekwa wazi kuanzia kuanzia tarehe 29 Aprili 2025kwa ajili ya wananchi kuhakiki taarifa zao, kurekebisha makosa yaliyojitokeza, pamoja na kuweka pingamizi dhidi ya majina yasiyostahili kuwepo.
Afisa huyo ameyasema hayo katika kikao maalum na wawakilishi wa vyama vya siasa kilichofanyika kwa ajili ya kujadili maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika kikao hicho, ilielezwa kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari litafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 7 Mei, 2025. Zoezi hili linalenga kuwawezesha wananchi waliotimiza umri wa kupiga kura, pamoja na wale waliopoteza au kubadilisha taarifa zao muhimu, kujiorodhesha na kusahihisha taarifa zao katika daftari hilo.
Vyama vya siasa vimeshauriwa kuhamasisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika hatua hii muhimu, ili kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki, na unaozingatia misingi ya kidemokrasia.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa