Pichani:Hali ya Ujenzi wa Jengo la Utawala,ikiwa ni moja kati ya Majengo katika Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kapalala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo hadi kufikia 11 Februari 2022.
Na: John Mganga DIO
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana unaoendelea katika Kata ya Kapalala Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo umeendelea kwa kasi ya kuridhisha huku Menejimenti ya Halmashauri ikifuatilia kwa karibu Maendeleo ya Ujenzi huo.
Hadi kufikia Tarehe 12, Februari 2022, Majengo yote katika mradi huo yameanza kupandishwa pasi kuwepo na changamoto yeyote inayoathiri Ujenzi huo ambapo shughuli za Ujenzi zimekua zikisimamiwa kwa karibu na Kamati ya Ujenzi ya Kata ya Kapalala ambayo wajumbe wake muda wote wameonekana wakiwa katika eneo la Ujenzi.
Tangu kuanza utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo Tarehe 5 Februari 2022 Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa sasa Bi. Tabia Nzowa kwa siku zote za wiki wametembelea eneo hilo kwa lengo la kujiridhisha na maendeleo ya Ujenzi wa mradi huo.
Pamoja na Wataalamu wengine,Februari 11, 2022 Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Elisonguo Mshiu alifika eneo la mradi kwa lengo la kukagua maendeleo ya Ujenzi na kuzungumza na Kamati ya Ujezi pamoja na Mafundi wazawa wanaotekeleza mradi huo kwa lengo la kubaini iwapo kuna changamoto yeyote katika eneo la Ujenzi kusudi ipatiwe ufumbuzi mara moja.
Bw.Mshiu amewahakikishia mafundi wanaotekeleza Ujenzi wa Mradi huo kuwa Halmashauri inafuatilia kwa karibu Ujenzi huo na kwamba Menejimenti inafanya ufuatiliaji kwa karibu zaidi ili endapo kutatokea changamoto yoyote basi ipatiwe ufumbuzi kwa wakati ili kutoathiri kasi ya Ujenzi huo.
Amewataka wajumbe wa Kamati ya Ujenzi ya Mradi huo kusimamia kwa karibu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mafundi ili kuhakikisha kuwa Mradi huo unakamilika kwa ubora ,viwango vinavyotakiwa na kwa wakati uliopangwa huku akiwataka kuelekeza nguvu kubwa zaidi katika kulinda vifaa vya Ujenzi vilivyopo katika eneo hilo la Ujenzi.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kapalala katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo unaotekelezwa kwa fedha za Mpango wa Kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari Nchini SEQUIP T unahusisha Vyumba Nane vya Madarasa,Maabara tatu,Jengo la Utawala,Maktaba moja,Chumba cha TEHAMA pamoja na matundu Ishirini ya Vyoo.
Serikali kupitia mpango wa kuinua Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP T ilitenga Kiasi cha Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya Ujenzi wa Sekondari hiyo ya Wasichana ambapo hadi sasa Shilingi Milioni 470 zimekwisha tolewa kwa ajili ya kutekeleza Mradi huo unaotarajiwa kukamilika ifikapo Tarehe 08, Agosti 2022.
Picha 1:Hali ya Ujenzi wa Jengo la Utawala katika Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kapalala hadi kufikia 11 Februari 2022.
Picha 2:Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bw.Elisonguo Mshiu akitoa maelekezo kwa viongozi wa Kamati ya Ujenzi ya Kata ya Kapalala alipofanya ukaguzi katika eneo la Mradi 11 Februari 2022
Picha 3;Hali ya Ujenzi katika moja kati ya Vyumba 8 vya Madarasa katika Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kapalala hadi kufikia 11 Februari 2022
Picha4;Hali ya Ujenzi wa moja kati ya Vyumba 3 vya Maabara katika Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kapalala hadi kufikia 11 Februari 2022
Picha 5;Stoo ya kuhifadhia Vifaa vya Ujenzi katika Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kapalala
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa