Pichani:Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiwa eneo la Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kapalala 07 Februari 2022 walipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo.
Na:John Mganga-DIO
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kapalala unaotekelezwa kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu ya Sekondari Nchini SEQUIP T katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo umeanza kutekelezwa kwa kasi nzuri na ya kuridhisha Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imejiridhisha.
Katika Ziara ya Wakuu wa Idara na Vitengo Nsimbo Tarehe 7 Februari 2022 kukagua maendeleo ya mradi huo walijiridhisha kuendelea kwa shughuli zote za Ujenzi ambapo Tayari vifaa mbalimbali vya Ujenzi ikiwemo matofari mchanga na kokoto vilikuwa eneo la mradi huku shughuli ya Uchimbaji wa Msingi kwa baadhi ya Majengo ukiendelea.
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ni moja kati ya Halmashauri Nchini zilizopokea fedha kwa ajili ya kutekeleza Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ambapo shilingi Milioni 600 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza Mradi huo ambapo mpaka sasa Halmashauri imepokea Shilingi Milioni 470.
Februari 3, 2022 kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Onesmo Buswelu katika Ziara yake kukagua Utekelezaji wa Mradi huo aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa namna ambavyo inatekeleza kwa wakati mradi huo ambapo alitoa rai kwa Menejimenti ya Halmashauri,Kamati za Ujenzi na Mafundi wanaotekeleza mradi huo kutekeleza mradi huo kwa uaminifu mkubwa na kuepuka mazingira yeyote yanayoweza kuathiri utekelezaji wa mradi huo.
Aidha DC Buswelu Amewataka Mafundi kuepuka kuhujumu vifaa vya Ujenzi na badala yake kutekeleza mradi huo kama yalivyo makusudi ya Rais Samia Suluhu Hassan huku akimtaka mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kupanga vizuri timu za usimamizi ili kuepuka kukwama kwa mradi huo.
Ameeleza kuwa ni muhimu kwa mafundi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na miundombinu muhimu kama Umeme ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza mradi huo usiku na mchana huku akimtaka Mhandisi wa Ujenzi Nsimbo kusimamia kwa karibu kazi hiyo kwa karibu zaidi.
Picha 1;Maandalizi ya kupandisha ukuta yakiwa yanaendelea hadi kufikia Tarehe 07 Februari 2022 katika Eneo la Kapalala ambako Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana unaendelea.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa