Madiwani katika Halmashauri ya Nsimbo wameonesha kuridhishwa na mchango wa wananchi katika utekelezaji wa miradi, huku wakisisitiza umuhimu wa serikali kuongeza juhudi katika kuiwezesha miradi hiyo. Aidha walimpongeza na kumshukuru Rais wa Tanzania Mh, DKT Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha ushirikiano na kuwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea.
Hayo yamesemwa Katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza katika mwaka wa fedha 2024-2025 kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Nsimbo. Madiwani waliwasilisha ripoti za kamati zao moja baada ya nyingine, huku wakikabiliwa na maswali mengi kutoka kwa wananchi. Wakuu wa idara walitoa majibu na maelekezo kwa kila swali lililoulizwa, jambo lililowezesha mazungumzo yenye tija na ya wazi.
Madiwani, hao kwa umoja wao wameomba serikali kutoa fedha za kukamilisha miradi hiyo na kuhakikisha nguvu za wananchi zinathaminiwa ipasavyo. Miradi iliyopendekezwa, ni pamoja na zahanati ya kalele, (Ugalla) shule ya msingi shikizi Kankosha iliyopo Ugalla na shule ya Sekondari ya Mnyamasi kata ya Ugalla, miradi hii imejengwa kwa juhudi za wananchi, lakini bado inahitaji rasilimali za serikali ili ikamilike kikamilifu.
Aidha, wamependekeza timu za wataalamu waendelee kushirikiana na wananchi kwa ukaribu ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa viwango vinavyostahili.
Katika tukio jingine Maafisa wa bonde wanaoshughulikia uhifadhi wa bonde Msaginya wanatakiwa kutoa elimu juu ya uhifadhi wa bonde kwa watumiaji ili waweze kulima ama kufanya shughuli za kibinadam kwa kufuata sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na si vinginevyo. Sheria ambayo inawataka kufuata umbali wa mita 60 kutoka kingo za mto. Hayo aliyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Stephano .B. Kaliwa wakati akijibu swali la Diwani wa Kata ya Machimboni lililouliza kuhusiana na katazo la kufanya shughuli karibu na mto alisema,
‘’Watu wa bonde Msaginya wapo kisheria hivyo watumiaji wanatakiwa kufuata sheria ya mazingira ya mwaka 2004 hivyo wanapotoka upande wa mto kwenda upande mwingine kwa ajili y shughuli za kibinadamu wanapaswa kuacha mita 60 na hii ni hata kwa wanyama sio kwa binadamu peke yake. Ikiwa kuna anayefanya hivi basi anavunja sheria. Ikiwa watu wa bonnde wataalikwa katika kikao cha Madiwani kama hiki ama katika vikao vya kamati basi watakuja na kutoa elimu hii muhimu.’’
Akiwasilisha taarifa ya kamati ya Elimu na Afya, Madiwani walitaka kupata ufafanuzi juu ya maboma ya zahanati,shule za msingi na sekondari ambazo hazijamalizika na zimejengwa kwa nguvu kubwa ya wananchi namna mikakati ilivyo katika kuaona maboma hayo yanapatiwa fedha ili kukamilika yaanze kutumika. alisema
‘’Kuna maboma yamejengwa kwa nguvu za wananchi, wadau na Halmashauri yenyewe,je ni lini ama ni utaratibu gani pengine umewekwa kuhakikisha maboma hayo yanamaliziwa ili wananchi waweze kupata huduma’’
Naye mwenyekiti wa kamati husika Mh Raphael Kalinga (Diwani wa kata ya Machimboni) akijibu swali hilo alisema, ofisi ya mipango tayari ipo katika hatua ya manunuzi ya vifaa kumalizia maboma hayo. Aidha alitoa ufafanuzi kua sio maboma yote yatakwisha kwa wakati mmoja ila ni kwa maboma matano ya shule kuzingatia kiasi cha fedha iliyotengwa cha sh milioni mia tatu thelathini na nane (338,000,000) kwa ajili ya kazi hiyo,
Madiwani wote kwa pamoja wameahidi kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo kwa karibu ili kuona kuwa jitihada za wananchi zinazingatiwa na kutambuliwa.
Kuhusiana na ukosefu wa maji katika zahanati amesema kua tayari Mkurugenzi Mtendaji kwa watawasilianana idara ya maji ya mkoa ili kuona namna changamoto hiyo itataatuliwa ili zahanati zipate maji.
Aidha ametoa agizo kwa Mkurugenzi kua wakati wa bajeti utakapofika atapaswa kupeleka mahitaji yoye ya maji ya shule na zahanati ambazo zinahitaji maji ili zitengewe bajeti katika idara husika. ili kuondoa sintofahamu ya kua bajeti haitoshi na kusiwepo na matatizo hayo, Alisisitiza kua Vyoo vilivyojengwa katiaka zahanati na shule zetu ni vizuri na vya kisasa hivyo ni vizuri vikawa na maji kwani vitasaidia watumiaji kuvitunza na kufaidi ubora wake.
‘’ ni vizuri serikali imejenga lakini kama havina maji havina faida’’sasa hii ni hasara maana fedha imewekwa sio mahali pake, alisema ‘’
Amemtaka Mkurugenzi mtendaji kufika katika zahanati kukagua mara kwa mara changamoto zitokanazo na maji ili kuwasaidia kina mama wanaojifungua na wagonjwa wengine, hoja ambayo ilipokelewa na kuwekwa katika hatua za utekelezaji.
Nae Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya Wilaya DKT Bonifas Masaga amesema kuwa kulikua na uhaba wa wataalamu wa Ultrasound hivyo wanatarajia kupata ajira mpya ambao watapelekwa katika vituo ambavyo kwa sasa vina changamoto hiyo.Alisema kuwa kwa sasa kutakuwa na huduma mkoba amao watakua wakihudumia katika vituo vianavyoonekana kua na uhaba wa wataalam huku wakisubiri taratibu zinazohusiana na ajira mpya zifanyike.Alisema hayo wakati akijibuswali lililohoji uhaba wa watumishi wa afya katika. Kata ya Katumba na Kanoge lililoulizwa na Diwani wa kata hizo
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri BW Halawa C.Malendeja. (Diwani wa kata ya Ugalla) alieleza kuhusu hali ya maendeleo katika sekta hizi muhimu. Baadhi ya maswali yalihusu upatikanaji wa vifaa vya elimu, changamoto za maji safi na salama, na upungufu wa wahudumu wa afya.Majibu yalitolewa na Madiwani wa kamati, wakieleza mipango iliyopo ya kushughulikia changamoto hizo
Katiaka uwasilishaji wa taariafa ya kamati ya ujenzi Madiwani pamoja na wananchi walitaka kujua maendeleo katika ujenzi wa barabara na mifumo ya maji taka. Maswali mengi yalihusu ubora wa miundombinu hiyo na lini miradi kadhaa itakamilika. Mwenyekiti wa kamati alitoa majibu na kueleza mpango wa kuharakisha ujenzi na ukarabati, akiahidi kushirikisha zaidi Na wadau wa barabara na wananchi katika hatua za maendeleo.
Katika hatua nyingine Baraza la madiwani limewathibitisha jumla ya watumishi (79) sabini na tisa wa kada mabalimbali ambao tayari walikua wamekidhi vigezo. Vilevile wapo watumishi (18) waliobadilishiwa kada na waliopandishiwa vyeo ni watumishi (125,000) mia moja ishirini na tano Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Halawa C Malendeja. alielekeza ofisi ya Mkurugenzi kuwa watumshi hao kuandikiwa barua kwa ajili ya kukamilisha utaratibu.
Nae Afisa Ustawi wa jamii Bi, Theresia Mwendapole alipata wasaa wa kuwajulisha Madiwani, na viongozi mbali mbali katika kutano wa madiwani kua tunapaswa kua na muda wa malezi kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka sifuri ya mimba mpaka miaka nane na kwamba kama mtoto wa miaka miwili atakosewa kwenye malezi itapelekea kuwa na watu ukubwani waliokosa vitu muhimu .Alisema hayo wakati akiwasilisha program mpya jumuishi ya makuzi na malezi na maendeleo ya awali ya mtoto ambayo ni mpya inayoratibiwa na TAMISEMI Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu. Pia program hii inaratibiwa na Wizara za kifedha.
Akihitimisha,Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye ni Diwani wa Kata ya Ugalla alisema kuwa, ni vizuri kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kwa kuwajali wananchi na kuonyesha tunaziona nguvu zao hasa katika miradi mikubwa walioianzisha. Ameeleza kua kuna miradi iliyofika hatua za mwisho kwa nguvu za wananchi pekee,na kuwa kile walichokianzisha wao ni dhahiri kua ndicho wanachokihitaji.Amesisitiza kua fedha zilizotengwa zisikae tuu benk bali ziwekwe kwenye utendaji ili nao waone umuhimu wa kazi zao walizofanya.sana alimshukuru Mh DKT Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi na kujitoa kwao na namna anvyotoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya wananchi.Amesisitiza kumuunga mkono kwa kua karibu na wananchi na kuzionyesha waziwazi nguvu zao kwa kufanya kazi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa