• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Viongozi,Watendaji Nsimbo wapatiwa mafunzo Mfumo wa Anuani za Makazi,Watakiwa kutanguliza Uzalendo wakati wa utekelezaji wa zoezi.

Imewekwa: February 15th, 2022

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Onesmo Buswelu akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Anuani za Makazi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Nsimbo Februari 15,2022

Nsimbo-Mtapenda

Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,Wakuu wa Idara na Vitengo,Madiwani , Watendaji wa Vijijiji na Kata pamoja na Wenyeviti wa Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,wametakiwa kuwa wazalendo na kutanguliza maslahi ya Taifa mbele wakati wa utekelezaji wa zoezi la uwekaji mfumo wa anuani za makazi.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu alipofungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo juu ya namna ya kutekeleza zoezi la uwekaji mfumo wa anuani za makazi.

DC Buswelu amesema  ili zoezi hilo liweze kutekelezwa kwa ufanisi ni vema Viongozi wakatimiza wajibu wao kwa kutoa ushirikiano wa kutosha ili kukamilisha zoezi hilo ambalo linafanyika Nchi Nzima.

Awali akitoa maelezo kuhusu Mfumo wa anuani za Makazi unavyofanya kazi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi Tabia Nzowa ameeleza kuwa Serikali imedhamiria kuweka Anwani za Makazi kwa nchi Nzima; ili kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishaji wa huduma katika maeneo mbalimbali.

 Bi Tabia ameeleza kuwa Mfumo wa anuani za makazi utatoa utambulisho wa mahali, mtu au kitu kilipo juu ya uso wa Nchi ambapo ametaja manufaa ya Mfumo huo kuwa ni pamoja na kuwezesha ufanyikaji wa baishara mtandao,kuboresha upataji,utoaji na upelekaji wa huduma na bidhaa mahala stahiki,kuimarisha ulinzi na Usalama,Uborshaji wa ukusanyaji wa mapato,kurahisisha shughuli za utafiti na upatikanaji wa Taarifa.

 Aidha Bi Tabia ameeleza kuwa Halmashauri inabeba jukumu la kupanga, kupima, kugawa, kumilikisha na kusimamia uendelezaji wa makazi na uundaji wa anwani utakaorahisha utambuzi wa maeneo ya Makazi, barabara na njia zinazowezesha kufika maeneo yote na hivyo kuwataka Viogozi na Wataalamu kushirikiana vema ili kufanikisha zoezi hilo.

Mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Maana ya Mfumo wa anuani za Makazi na Postikodi,Utambuzi wa Barabara na Ugawaji wa Namba,Uwekaji namba kwenye makazi,Aina za Vibao kwenye nyumba na barabara,namna ya kutumia na kuingiza Taarifa kwenye Mfumo,pamoja na Mafunzo kwa Vitendo ambapo Washiriki walitembelea maeneo mbalimbali ya Mitaa kwa lengo la kujifunza kwa vitendo namna ambavyo vibao vya barabara na mwenye nyumba vitawekwa.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WANANCHI NSIMBO WATAKIWA KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

    May 01, 2025
  • WAFANYAKAZI WAPEWE MOTISHA KAZINI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI NSIMBO LARIDHISHWA NA MIRADI YA MAENDELEO

    April 30, 2025
  • KAMISHNA WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA MAFUNZO YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI VYA BAYOMETRIKI (BVR KITS) KATIKA JIMBO LA NSIMBO

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa