Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwamvua Mrindoko, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), akisisitiza umuhimu wa kutoa heshima kubwa kwa wafanyakazi ili kuongeza ari na motisha kazini. Amesema kutambua mchango wa wafanyakazi ni njia madhubuti ya kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Mhe. Mrindoko amesisitiza kuwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanapaswa kushirikiana na Serikali katika kuboresha ustawi wa wafanyakazi nchini. Amesema anawapongeza watumishi kwa bidii na uadilifu katika utendaji kazi, na kuwataka waendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kuwa wao ndio mashuhuda wa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutoa fedha za maendeleo, ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi trilioni 1.3 zimetolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na malipo ya posho, likizo na mafao ya wafanyakazi, kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkurugenzi Mtendaji, wakuu wa idara na watumishi wamehudhuria kwa pamoja, wakionesha mshikamano na uzalendo.
Maadhimisho hayo pia yamehusisha utoaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka sekta mbalimbali, kama ishara ya kutambua mchango wao katika maendeleo. Baadhi ya wafanyakazi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamepokea tuzo, ikiwa ni sehemu ya kutambua utendaji wao bora katika Mkoa wa Katavi na Taifa kwa ujumla.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa