Wananchi katika Halmashauri Nsimbo, wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupanda miti na kuitunza ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira. Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa ya Nsimbo ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mhe. Jamila Yusuph katika maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika. Katika kilele Cha maadhimisho hayo amewahimiza Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kujenga tabia ya kupanda miti pamoja na kuitunza. "Natoa wito kwa Taasisi zote zilizopo Halmashauri ya Nsimbo kuhakikisha wanapanda miti Katika maeneo yao", Amesema Afisa Tarafa.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Watumishi wote wa Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa vyama vya Siasa, Wanafunzi, asasi za kiraia na makundi mbalimbali. Sherehe za maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru zimehitimishwa kwa michezo mbalimbali iliofanywa kabla ya Disemba 09 ikiwemo midahalo na mabonanza mbalimbali.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa