Pichani:Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Paul Sheyo akizungumza na Wakazi wa Kijji cha Mtambo kwenye mafunzo ya mbinu bora za Kilimo cha zao la Pamba wakati wa Hamasa ya zao hilo.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamehimizwa kuachana na kilimo cha mazoea na badala yake kutumia mbinu bora na za kisasa kulima zao la kimkakati la Pamba ili kujikwamua na umasikini.
Katika Kampeni endelevu ya Hamasa kwa wananchi kutumia mbinu bora na za Kisasa za kilimo cha zao la pamba,Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Nsimbo Bw.Paul Sheyo amewaambia kwa nyakati tofauti Wananchi hususani wanaojihuisha na Shughuli za Kilimo cha Pamba kuwa njia pekee ya kuepuka Hasara ni kuachana na kilimo cha mazoea na badala yake kutumia mbinu bora na za kisasa zinazoelekezwa na wataalamu wa Kilimo cha Pamba ili kuleta tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Amesema ni vema Wakulima wakasikiliza na kuzingatia ushauri wa Kitaalamu wakati wa kullima zao hilo kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kwa sehemu kubwa kuongeza uzalishaji kwa kuwa Pamba itasitawi kama ilivyokusudiwa.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa