Kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2025, Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata katika Jimbo la Nsimbo Mkoani Katavi wamepewa mafunzo elekezi yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani humo. Akifungua mafunzo hayo, msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Nsimbo Bwana Julias Zakaria Moshi amewataka wasimamizi wasaidizi hao kufuata Sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Bwana Moshi amewakumbusha wasimamizi hao wasaidizi ngazi ya Kata kufuatilia kwa umakini mafunzo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili wawe watendaji wazuri na waendelee kuwa wazalendo, waaminifu na kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata viapo vyao kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha, amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa, sheria, kanuni na maelekezo mbalimbali ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Sambamba na hayo, Bwana Moshi amewataka wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata kusoma kwa makini Katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na kuuliza ili kupata ufafanuzi wa jambo lolote litakaloonekana kuwa na changamoto katika utekelezaji wa majukumu waliyopewa.
Kabla ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo, Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata wamekula kiapo cha kutunza siri na kujivua uanachama kwa waliokuwa wanachama wa vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu 2025
Itakumbukwa kwamba, Tuma Huru ya Tiafa ya Uchaguzi imetangaza Siku ya Jumatano ya taerehe 29/10/2025 kuwa siku ya Uchaguzi mkuu, ambapo watanzania wenye sifa watatumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua Rais, wabunge na madiwani.
KURA YAKO HAKI YAKO, JITOKEZE KUPIGA KURA
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa