Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamepongezwa kwa jitihada mbalimbali walizofanya kufanikisha shughuli mbalimbali za maandalizi na mapokezi na hatimae makabidhiano ya mbio za Maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Salehe Msompola wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani kufunga Hesabu za Mwaka wa fedha 2020/2021.
Makamu Mwenyekiti Msompola amesema Mafanikio yaliyopatikana ya kufanikisha mapokeziz ya mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2021 ni matokeo ya Watumishi waliounda Kamati mbalimbali kutekeleza kwa moyo mmoja na kwa uzalendo Majukumu mbalimbali waliyopangiwa na Mwenyekiti wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Bi Jamila Yusuph Kimaro.
Kwa Upande wake Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambae amekaimu Nafasi ya ukurugenzi katika kikao hicho Malaumu cha Baraza la Madiwani Bi.Tabia Nzowa licha ya pongezi alizotoa amewataka Watumishi kutumia changamoto chache zilizojitokeza kujipanga vyema kwa ajili ya shughuli nyingine zijazo za Mwenge wa Uhuru pamoja na Shughuli nyingine za Kitaifa kwakurekebisha changamoto hizo kusudi waweze kufanya vizuri zaidi.
Mwenge Maalumu wa Uhuru uliwasili na kupokelewa Nsimbo 24,Septemba 2021 ambapo ulizindua vyumba viwili vya Madarasa pamoja na kuweka Jiwe la Msingi kituo cha Mafuta kilichopo Eneo la Isinde.
Aidha Mwenge Maalumu wa Uhuru ulizindua Kablu ya kupinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Nsimbo na baadae kuelekea katika Viwanja vya Mkesha katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashato na baadae kukabidhiwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika siku ya Tarehe 24 Septemba 2021.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa