Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameshauriwa kufanya kazi kwa Weledi, kujitolea na uzalendo ili wawe Mashujaa katika maeneo yao ya kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Ndg. Anthony Andrew Geay katika kuadhimisha siku ya Mashujaa waliopambana kupata Uhuru wa Tanganyika Nchini. Anthony amesema katika siku hii ya Mashujaa walifariki katika vita ya Kagera ya Mwaka 1978-1979.
Naye Afisa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Archileus Bushaijabwe amesema katika kuadhimisha siku ya mashujaa wametekeleza Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Kwa kufanya Usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.
Amesema wamechagua kufanya usafi Hospitali kutokana na watu wengi kufika katika eneo hilo, hivyo linatakiwa liwe safi.
Tarehe 25/07/2023 ni siku maalum ambayo Tanzania tunaazimisha na kuwakumbuka Mashujaa wetu waliopigania Maslahi ya Taifa hili katika Nyanja Mbalimbali kwa Uzalendo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa