• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

MKUU WA WILAYA YA MPANDA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA BARABARA KIJIJI CHA IKONDAMOYO.

Imewekwa: October 22nd, 2024

Mkuu wa Wilaya Bi Jamila Yusufu Kimaro amezindua rasmi mradi wa Uboreshaji wa Miundombunu ya Barabara katika Halmashsuri ya Nsimbo. Mradi huo unahusisha uboreshaji wa barabara  za Ikondamoyo – Mihambo Usense Km 6.0, Urwira – Mission B Km 6.0, Songambele – Mkumbi Road Km 5.0 na Nyati Km 1.5, pamoja na  Ujenzi wa Daraja la Upinde la Mawe katika barabara ya Ikondamoyo – Mihambo – Usese na Ujenzi wa Makaravati  kwenye Barabara Za Urwira – Mission B (5), Songambele – Mkumbi Road (5) Na Barabara Ya Nyati (3).

Akizungumza  katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya alieleza umuhimu wa barabara hiyo kwa maendeleo ya kijiji, akibainisha kuwa mradi huo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kuimarisha miundombinu vijijini Alisistiza kua barabara hiyo itachochea uchumi wa wananchi kwa kurahisisha usafiri na biashara. Vilevie  alimpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha, nyingi kwa ajili ya mradi huu ambapo kila mtu anaona kwa macho serikali sikivu yenye kujali wananchi wake.

Aidha Mkuu wa Wilaya  Aliongeza kua Serikali imeendelea kuweka kipaumbele katika kuboresha maisha ya wananchi, hususan katika maeneo ya vijijini, na amekiri  TARURA kupokea kiasi cha Sh 838’426’765.00 kwa ajili ya mradi huo  Aliongeza kua hadi  kufikia tarehe 29/04/2025 ikiwa ni miezi sita tangu kuanza kwa mradi huo, uwe umekamilika

Katika hatua nyingine muhimu Mkuu wa wilaya alisaini mkataba wa ujenzi na kukabidhiwa rasmi kwa mkandarasi atakayesimamia mradi  huo ambapo  Katika tukio hilo, alimkabidhi  cheti rasmi cha kutekeleza mradi huo.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa wilaya aliambatatana na viongozi wa  chama,Madiwani afisa Tarafa. Viongozi hawa walitoa shukrani za dhati kwa serikali  kwa jitihada zake za  kuboresha miundo mbinu. Na kusistiza wananchi kushirikiana vizuri na Mkandarasi ili kufanikisha mradi huo.

Kwa upande wa ajira za vijana, Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa vijana wa kijiji kushiriki kikamilifu katika kazi za ujenzi wa mradi huo kwa uaminifu na bidii. Alisema kwamba ajira hizo ni fursa muhimu kwa vijana kujiendeleza kiuchumi, na aliwasihi kufanya kazi kwa uwajibikaji ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa viwango vya juu. na kwa wakati

Akizungumza kuhusu mchakato wa uchaguzi, Mkuu wa Wilaya aliwakumbusha wananchi kuhusiana na uchaguzi kwa kusema kua,‘’zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi limekamilika, na sasa ni muda wa kuelekea kwenye uchaguzi wenyewe. Mnapaswa kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo kwa vitendo badala ya kupelekwa na maneno matupu ya wagombea. ninyi wenyewe ni mashuhuda wa maendeleo  yanayofanywa na serikali’’ alisema haya akisisitiza umuhimu wa kuchagua kwa busara na kwa kuzingatia uwezo wa mgombea kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma’’.

Aidha msimamizi wa mradi huo ambaye na meneja wa TARURA Mpanda, wakati wa kuwasilisha mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo aleleza mkataba huo unaweka misingi wa utekelezaji wa mradi na kwa kuzingatia manunuzi ya serikali ambappo mkataba huo ulisainiwa na mkuu wa wilaya  mbele ya washiriki wa mkutano huo. Alitoa wito kwa Mmkandarasi kuhakikisha kwamba ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika ili kulinda thamani ya fedha za umma kama zilivyotolewa kwenye mradi huo.

Nae mkandarasi  aliyejulikana kwa jina M/S/SABD COMPANY LMTD  aliyekabidhiwa mradi huo alishukuru serikali kwa kuendelea kumuamini aliwaomba wananchi kwa ushirikiano  na  kuwataka wawe kipaumbele katika kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa  kisha alimpongeza Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kwa miundombinu. Aliahidi kufanya kazi kwa kasi na ubora ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha wananchi wote.

Wananchi walionyesha shukrani zao kwa serikali kwa kuwajali na kuwaletea maendeleo, huku wakiahidi kushirikiana kikamilifu na mkandarasi ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa mafanikio.makubwa.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa