• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Mpango harakishi na Shirikishi wa Utoaji Chanjo ya UVIKO 19 wazinduliwa Nsimbo,Wengi wajitokeza kuchanjwa.

Imewekwa: October 4th, 2021

Pichani:Wananchi katika Kata ya Kanoge wakiwa wamepanga foleni  kwa ajili ya kupata chanjo ya UVIKO 19 wakati Mtaalamu wa Afya kutoka Kituo cha Afya Kanoge akiendelea kuwapatia Chanjo.

Idadi kubwa ya Wananchi katika  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 wakati wa Uzinduzi wa Mpango harakishi na shirikishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 uliofanyika katika Kata ya Kanoge katika viwanja vya  Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Kanoge Tarehe 03 Septemba 2021.

Muitikio huo mkubwa wa Wananchi kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19   ni matokeo ya nguvu kubwa kutoka kwa Wataalalmu wa Afya Nsimbo (CHMT) iliyoelekezwa katika kutoa Elimu na Hamasa kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kupata Chanjo ya UVIKO 19.

Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mpango Harakishi na Shirikishi wa utoaji wa Chanjo ya UVIKO 19 Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kanoge  Bw.Salehe Msompola amewaambia Wananchi wa Kata ya Kanoge kuwa ni muhimu kupata chanjo ya ya UVIKO 19 ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza endapo mtu hatapata chanjo ya hiyo.

Makamu Mwenyekiti huyo amewataka Wananchi kupuuza uzushi unaoenezwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao kisiasa kuwa chanjo hiyo si salama kwa matumizi ya binadamu na kwamba  ni njama za Wazungu  kuwaangamiza Waafrika Duniani na badala yake Wananchi kujikita zaidi kusikiliza maelekezo ya Wataalalmu wa Afya Nchini.

Msompola ameongeza kuwa endapoio Jamii ya Kitanzania itahamasika kupata chanjo ya UVIKO 19 itasaifia kwa kiasi ikubwa kupunguza na kuondoa kabisa Ugonjwa wa UVIKO 19 na kwamba Taifa litarejea katika hali ya kawaida na Wananci watapiga hatua kimaendeleo huku akiataka waliokwisha chanja UVIKO 19 kuwa mabalozi kuwahamasisha wengine ili waweze kupata chanjo hiyo.

Akiwasilisha Taarifa ya hali ya Utoaji wa chanjo ya UVIKO19  katika Halmashaurii ya Wilaya ya Nsimbo,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Ismail Kanani amesema Halmashauri imepokea dozi 1700 kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya makundi maalumu na makundi ya kipaumbele na kufuatiwa na watu wenye umri kuanzia miaka 18.

Ameyataja makundi ya kipaumbele kuwa ni Watumishi wa Afya,Skta ya Utalii,Walimu pamoja kundi la watu wanaosumbuliwa na magonjwa Sugu ikiwemo Sukari,Magonjwa ya Moyo nk.

Mganga Mkuu Kanani ameeleza kuwa mara baada ya kupokea dozi hizo za chanjo Halmashauri ilizindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo kwa makundi maalumu katika kituo cha Afya Katumba ambapo vituo vingine viwili ambavyo ni kituo cha Afya Kanoge na Kituo cha Afya Mtisi viliandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma za chanjo ya UVIKO 19.

Ameeleza kuwa hadi sasa huduma ya chanjo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inaendelea kutolewa katika vituo 21 vya kutolea huduma za afya ambapo watu 946 kati yao Wanaume 554 na wanawake 392wamepatiwa chanjo ya UVIKO 19 ambapo mpaka hivi sasa hakuna kisa chochote kuhusu madhara makubwa ya chanjonya UVIKO 19, isipokuwa maudhi madogomadogo  yanayotokea kaa ilivyo katika matumizi ya dawa nyinginez za binadamu.

Mpango harakishi na shirikishi wa utoaji wa Chanjo ya UVIKO 19 unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo kampeni na Hamasa vinaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata chanjo ya UVIKO 19.





Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa