• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Naibu Waziri Gekule apongeza jitihada za Mbunge kuinua Michezo Nsimbo.

Imewekwa: September 13th, 2021

Pichani:Naibu Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari Utamaduni Wasanii na Michezo Mh.Pauline Gekule akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kanoge 13 Septemba 2021

Naibu Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari Utamduni Wasanii na Michezo Mh.Pauline Gekule amempongeza Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe kwa jitihada mbalimbali anazofanya kuinua Sekta ya Michezo ndani ya Halmashauri.

Mh.Gekule ametoa pongezi hizo alipozungumza na Wananchi wa Kata ya Kanoge Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika Shughuli ya kukabidhi Vikombe na zawadi mbalimbali kwa Washindi waliofuzu  Ligi ya Anna Lupembe ambapo timu 132 ndani ya  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo zinashiriki  katika ligi hiyo katika  ngazi mbalimbali ambapo pia timu 28 za mpira wa Miguu za Wavulana na Wasichana kwa  Shule za Sekondari  zimezinduliwa kushiriki katika Ligi ya kuwania  Kombe la Anna Lupembe kwa Shule za Sekondari

Naibu Waziri Gekule amewaambia Wananchi wa Kata ya Kanoge Nsimbo kuwa kuanzishwa kwa Ligi ya  Kombe la Anna Lupembe kumesaidia kwa sehemu kubwa kuibua vipaji mbalimbali katika Michezo na hivyo kuifanya Sekta ya Michezo Nsimbo kupiga hatua kubwa kimaendeleo,ambapo amewataka Wananchi pamoja na Wadau mbalimbali wa michezo Mkoani Katavi kuiga mfano wa Mh.Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe katika jitihada za kuinua Michezo Nchini

Awali katika Kikao na Maafisa Habari Utamaduni na Michezo wa Mkoa wa Katavi Naibu Waziri Gekule ameeleza kuwa anatambua changamoto ya uhaba wa watumishi katika Kada za Michezo utamaduni na Habari ambapo  amehimiza uwajibikaji kwa waliopo ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Wasanii Utamaduni  na Michezo Katavi inaendelea huku akiahidi kutatua changamoto ya Uhaba wa Mafaisa Michezo na Utamaduni mkoani humo.j

Akitoa salamu kwa Wananchi mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe amesema lengo la Ligi hiyo ni kuibua vipaji na kuleta ari ya Michezo ndani ya Halmashauri jambo litakalosaidia kwa sehemu kubwa kuibua vipaji mbalimbali vya Wanamichezo katika Jimbo lake.

Mh.Lupembe amemuambia Naibu Waziri Pauline Gekule kuwa kuanzisha Ligi hiyo katika  Halmashauri imetokana na Halmashauri kuwa nyuma katika michezo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Maafisa Utamaduni na Maafisa Michezo jambo ambalo limekuwa likiathiri kwa sehemu kubwa uratibu wa Ligi mbalimbali Nsimbo.

Amesema kuanzishwa kwa Ligi ya Anna Lupembe ni utekelezaji wa kile alichokiahidi wakati akiinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu Sekta ya Michezo na kwamba Wananchi watarajie yote yaliyoahidiwa katika Sekta hiyo ya michezo yatatekelezwa.

Aidha Mh.Mbunge Lupembe amesema Ligi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu baadhi ya Wachezaji wenye vipaji vikubwa walioibuliwa katika Ligi hiyo wameweza kuchukuliwa kwenda kushiriki michuano katika sehemu mbalimbali nje ya mkoa wa Katavi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani amempongeza Mbunge wa Nsimbo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza sekta ya Michezo ndaniya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Zawadi mbalimbali ikiwemo Mipira na Jezi pamoja na Makombe vyenye thamani ya Shilingi Milioni tatu zimetolewa kwa Washindi mbalimbali walioshiriki na kufuzu Ligi hiyo ya Kombe la Anna Lupembe

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa