• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Nsimbo DC yatolea Ufafanuzi madai kukwama Mradi wa Ujenzi Kituo cha Afya Ugalla

Imewekwa: March 15th, 2022

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mhandisi Martin Kasonso akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mh.Jamila Kimaro alipotembelea Kituo cha Afya Ugalla 14 Machi Machi 2022 kujionea maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo.


TAARIFA KWA UMMA


Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imesikitishwa na Habari za uongo zenye viashiria vya nia ovu zilizosambazwa kupitia makundi mbalimbali ya Watsup pamoja na Mitandao ya kijamii zilizochapishwa na Mwandishi wa Habari wa Blogu ya Katavi kwanza zikielezea madai ya kusimama kwa ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Afya Ugalla kwa Muda wa Wiki mbili pamoja na madai ya Mkandarasi kutolipwa kwa muda wa wiki mbili.

Habari hizo zilichapishwa kupitia Blogu ya Katavi Kwanza katika chapisho lake la Tarehe 13 Machi 2022 zikimnukuu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katambike  akisema Ujenzi wa kituo cha Afya Ugalla umesimama kwa takribani wiki mbili.

Katika chapisho jingine Mwandishi wa Blogu ya Katavi kwanza alichapisha habari katika Blogu yake hiyo ikimnukuu Mwenyekiti wa Kijiji cha Katambike akisema Mkandarasi anayejenga Mradi huo hajalipwa fedha zake kwa muda Mrefu jambo lililopelekea kusimama kwa mradi huo.

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inalaani vikali kitendo cha kusambaza Habari  hizo zisizo na ukweli wowote zenye viashiria vya nia Ovu ya kuichafua Taswira ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kilichofanywa na Mwandishi wa Habari wa Blogu ya Katavi kwanza kwa maslahi yake binafsi  na kwamba inatoa onyo kali kwa Mwandishi huyo wa Habari.

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inaujulisha Umma wa Watanzania kuwa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Ugalla haukusimama kama ilivyoelezwa na Mwandishi wa Blogu ya Katavi kwanza na badala yake shughuli zote za Ujenzi zilikuwa zikiendelea kwa Takribani wiki mbili zilizopita hadi hatua ulipofikia mradi huo.

Ukweli ni kuwa katika Hoja ya kwanza  Ujenzi wa Kituo cha Afya Ugalla mpaka hatua ulipofikia  umetekelezwa kwa kipindi cha wiki tatu.Hadi kufikia 04 Machi 2022 na kwamba katika kipindi hicho shughuli mbalimbali za Ujenzi zilikuwa zikiendelea

Katika Hoja ya Pili ukweli ni kuwa Ucheleweshaji wa Malipo ya Mzabuni wa kusambaza mchanga,Mawe na Kokoto ulisababishwa na kamati ya Ujenzi ya Kituo hicho kutaka mzabuni alipwe fedha nyingi kuliko kiasi cha malighafi zilizofikishwa katika eneo la mradi jambo lililopelekea  wataalam kujiridhisha na mzigo uliofika kabla ya kufanya malipo.

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inatoa wito kwa Waandishi wa Habari kote Nchini kuzingatia misingi ya taaluma yao ya Uandishi wa Habari ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Habari zinatolewa  kwa kuzingatia  usawa ikiwa ni pamoja na kujiridhisha na pande zote mbili kabla ya kusambaza  na kwamba haitosita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale wote watakaosambaza Habari za Uongo  dhidi ya Halmashauri.

Aidha Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji inawahakikishia  Wanahabari kote Nchini kuwa itaendelea kutoa  ushirikiano wa kutosha kwa jambo lolote linalohitaji Ufafanuzi  wa Kitaalamu kwa Waandishi wa Habari lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata haki yao ya msingi ya  Taarifa sahihi na kwa wakati pindi inapohitajika.

Imetolewa na;

 

 

John A.Mganga

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa