• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Nsimbo yakamilisha Ujenzi,yakabidhi vyumba 87 vya Madarasa kwa RC Katavi.

Imewekwa: January 10th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hoza Mrondoko(Kulia mwenye kilemba chekundu) akizundua moja kati ya vyumba 87 vya Madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Sitalike  Mradi ambao umekamilika kwa asilimia 100 hadi kufikia Desemba 31 2021.


Na:John Mganga DIO

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kusimamia kikamilifu na kufanikisha Utekelezaji wa Miradi inayotekelezwa kupitia Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Mh.Mrindoko ametoa  pongezi hizo katika Hafla ya Uzinduzi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Sitalike  kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kukamilisha Ujenzi kwa asilimia 100  vyumba vya Madarasa 87 pamoja na kukamilisha Utengenezaji wa  Madawati 470,pamoja na viti na meza 1153.

 Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed  Ramadhani   mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati wa Hafla ya kukabidhi miradi hiyo,ilieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilipokea Shilingi  1,740,000,000.00  kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 87 vya Madarasa katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari ambapo Ujenzi huo  ulikamilika kwa asilimia 100 hadi kufikia 31 Desemba 2021.

Mkurugenzi Mohamed alieleza kuwa kwa sekta ya Elimu Sekondari Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 860,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa katika shule 12 za sekondari pamoja na utengenezaji wa viti na meza 2,150 ambapo kwa sekta ya Elimu Msingi Halmashauri ilipokea kiasi cha Tshs. 880,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 44 vya madarasa katika vituo shikizi 11 pamoja na utengenezaji wa madawati 660.

Kiasi cha Shilingi Milioni Thelathini na Saba Mia Saba Ishirini na Saba Elfu, Mia nne sitini na mbili (37,727,462.05) kimebaki ikiwa ni kwa ajili ya fedha ya matazamio za mafundi Tshs. 18,878,098.00, utengenezaji wa madawati ni Tshs. 12,506,525.00 na malipo ya vifaa vilivyoongezeka ni Tshs. 6,342,839.05.

Aidha Halmashauri imebakiwa na vifaa vyenye thamani ya Tshs. 29,117,000.00 ambavyo baadhi vitatumika kujengea vyoo katika vituo shikizi ili shule ziweze kusajiliwa na baadhi vitabadilishwa ili kugharamia utengenezaji wa madawati, viti na meza kwa shule ambazo hazijakamilisha.


MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA



Picha 1:Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya UVIKO 19 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Hoza Mrindoko 10 Jaanuari 2022

 


Picha 2;Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko kwa kutambua mchango wake wa usimamizi makini wa miradi ya UVIKO 19.

Picha 3; Mmoja wa wakuu wa Shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kenswa  Aidan Killo akipokea Cheti cha kutambua Mchango wake wa usimamizi makini wa miradi ya UVIKO 19

Picha 4;Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Salehe Msompola akipokea cheti cha kutambua mchango wa usimamizi makini wa Miradi ya UVIKO 19 kwa niaba ya Mwenyekti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Halawa Charles Maelendeja.


Picha 5;Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko akitoa hotuba wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Madarasa ya UVIKO 19 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa