• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU JANUARY-MACHI, 2023.

Imewekwa: March 31st, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imekua ikitekeleza afua mbalimbali za Lishe kwa kufuata mwongozo wa Taifa wa Lishe, Mpango jumuishi wa Taifa wa pili (2021/2022-2025/26) pamoja na sera mbalimbali za nchi zinazolenga kuzuia na kupambana na Udumavu na Utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka 5.  Pia kuzuia na kupambana na matatizo yatokanayo na ulaji usiofaa kwa watu wazima kama vile Saratani, Kisukari, Magonjwa ya mfumo wa damu (Cardiovascular diseases) na Shinikizo la damu hasa katika maeneo yale ya kipaumbele yaliyopo katika mkataba wa lishe ngazi ya Halmashauri, Kata na kijiji.

Katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri imefanya shughuli za usimamizi elekezi ambazo ni kuangalia utoaji wa Elimu ya Lishe katika vituo vya kutolea Huduma za Afya, Utambuzi na Matibabu ya Utapiamlo Mkali, utumiaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu na Upimaji wa hali ya Lishe kwa Watoto wa  chini ya miaka Mitano.

Sanjari na hayo, umefanyika pia uhamasishaji wa utoaji wa chakula shuleni kupitia mikutano ya Hadhara iliyoendeshwa na watendaji wa vijiji na Kata ambapo wazazi walielezwa faida za wanafunzi kupata chakula shuleni na jinsi itakavyosaidia kupunguza utoro, uachaji shule na namna itakavyosaidia kukuza kiwango cha ufaufalu kwa  wanafunzi. Pia afisa Lishe wa Halmashauri ya Nsimbo  ametembelea Shule ya sekondari Mkaso, na Shule za Msingi za Isanjandugu, Songambele na Nsimbo kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za Lishe katika shule hizo ili wanafunzi hao wafahamu Lishe bora na umuhimu wa kula vyakula mchanganyiko ili waweze kuwa mabalozi wa Lishe bora kwenye jamii na familia zao.

Aidha Halmashauri kupitia Sehemu ya huduma za lishe kwa kushirikiana na kitengo cha mawasiliano serikalini kimeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kufikisha Elimu ya Lishe kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa kuandaa Makala laini na ngumu za lishe pamoja na vipeperushi vya makundi matano ya vyakula na kuvisambaza kupitia tovuti ya Halmashauri na mitandao ya kijamii, pia kutumia radio zilizopo Mkoa wa Katavi kutoa elimu ya Lishe bora.


Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa