• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Wazee Maarufu,Viongozi wa Dini Katavi Wamshukuru Rais Samia, RC Katavi awataka kuwa mabalozi kueleza mafanikio ya Fedha za UVIKO 19.

Imewekwa: January 13th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua  Hoza Mrindoko akizungumza na wazee maarufu na viongozi wa Dini wa Mkoa wa Katavi  aliokuwa ameambatana nao alipotembelea Shule ya ya Sekondari Uruwira kukagua Madarasa ya UVIKO 19 yaliyokabidhiwa  10,Januari  2021.


Na; John Mganga -DIO

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Hoza  Mrindoko amewataka Wazee Maarufu na Viongozi wa Dini Mkoani Katavi, kuwa mabalozi kwa Wananchi  katika kutangaza mazuri yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Samia ikiwemo mafanikio yaliyopatikana kutokana na fedha zilizotolewa kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo 13 Januari 2022 katika Ziara yake akiambatana na Viongozi wa Dini na Wazee maarufu wa Mkoa wa Katavi kukagua Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Uruwira katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Mh.Mrindoko amewaambia Wazee maarufu na viongozi wa Dini kuwa, Mkoa wa Katavi katika kipindi kifupi cha awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kufufua uchumi katika  Sekta mbalimbali Nchini ulioathirika kutokana na   mawimbi kadhaa ya Janga la UVIKO 19, mkoa umepokea zaidi ya Shilingi Bil 32 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 425 katika Shule za Msingi na Sekondari,Vituo Shikizi,Utengenezaji wa Viti na meza  pamoja na Uboreshaji wa miundombinu katika Sekta ya Afya.

Aidha Mh.Mrindoko amewapongeza Viongozi mbalimbali walioshiriki katika usimamizi mpaka kumaliza Ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo pia amewataka kutumia muda aulioaki kuhakikisha kuwa Wanahamasisha wazazi kuwaandikisha watoto wenye sifa za kujiandikisha Darasa la awali ili waweze kupata haki yao ya Elimu kwa kuwa Serikali imetekeleza kikamilifu wajibu wake wa kuhakikisha uwepo wa Vyumba vya madarasa pamoja na madawati.

Wakizungumza mara baada ya  kukagua Vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Uruwira   vilivyojengwa kupitia fedha za UVIKO 19 vyenye thamani ya Shilingi Mil.80, viongozi mbalimbali wa dini pamoja na Wazee maarufu  wa Mkoa wa Katavi wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo   kwa namna ambavyo imesimamia  Ujenzi wa Miundombinu hiyo hadi kukamilika kwa wakati.

Aidha Viongozi hao wa Dini  pamoja na Wazee Maarufu wamemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh.Samia Suluhu Hassan kwa jitihadambalimbali anazofanya katika kuhakikisha kuwa anafufua Uchumi na Sekta mbalimbali zilizoathiriwa na Janga la UVIKO 19 huku wakiahidi kuwa mabalozi kuyatangaza mafanikio hayo kwa Wananchi.

 Mashaka Nassor Kakulukulu,Sheikh wa Mkoa wa Katavi  ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo imefanikisha utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa ubora wa hali ya juu na kueleza kuwa jambo hilo ni kiashiria kuwa fedha iliyotolewa imetumika kikamilifu.

“Hakuna Ushahidi Mzuri kama ushahidi wa kujionea,tumekuja kujionea namna ambavyo miradi hii imetekelewa kwa fedha za Fedha za IMF na kwa kuwa tumejionea kila mtu anaona wazi kuwa kazi imefanyika kikamilifu, watoto wetu zamani walisoma katika vyumba ambavyo havikuwa vizuri lakini sasa hivi tunajionea vyumba vimekamilika kwa ubora wa ahali ya juu na watoto watasoma vizuri”alaisema Sheikh Kakulukulu.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Moravian Mpanda Mjini Ernest Simpanzye amesema ni vema wananchi wakatambua kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kuwa inafufua sekta zilizoathiriwa na Janga la UVIKO ambapo licha ya Kumshukuru na kumpngeza Rais Samia amewataka Wananchi kumuuunga mkono katika mambo yote ya kimaendeleo anayolifanyia Taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe amempongeza Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Fedha nyingi kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba Nsimbo imeshuhudia mapinduzi makubwa kimaendeleo katika awamu hii ya sita.

Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ilikamilisha Ujenzi wa Vyumba 87 vya Madarasa hadi kufikia 31 Desemba 2021 na kukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi vyumba hivyo 10 Januari 20211 ambapo kazi hiyo imekamilika kwa asilimia 100.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA.

Picha 1:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko(Mwenye Ushungi Mweusi) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mohamed Ramadhani pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Nsimbo mara baaada ya kuwasili Shule ya Sekondari Uruwira katika ziara yake akiambatana na Viongozi wa Dini na Wazee maarufu wa Mkoa wa Katavi.


Picha 2:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Wazee Maarufu pamoja na viongozi wa dini(Hawapo pichani)katika moja ya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO 19 katika ziara yake Shule ya Sekondari Uruwira kukagua miradi hiyo akiambatana na Wazee maarufu na viongozi wa Dini.

Picha 3;Wazee Maarufu pamoja na Viogozi wa Dini wa Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mh.Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara baada ya ukaguzi wa majengo ya UVIKO ndani ya moja kati ya vyumba vya madarasa ya UVIKO yaliyokamilika  katika Shule ya Sekondari Uruwira.


Picha 4;Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Anna Richard Lupembe akitoa salamu za Shukrani kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan  katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi  kukagua miradi ya UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.

Picha 5;Sheikh wa Mkoa wa Katavi  Mashaka Nassor Kakulukulu akizungumza kwa niaba ya Viongozi wa Dini mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa ya UVIKO 19 yaliyokamilika katika shule ya Sekondari Uruwira katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akiambatana nao kukagua miradi hiyo.


Picha 6;Mchungaji wa Kanisa la Moravian Mpanda Mjini Ernest Simpanzye akitoa salamu za shukrani wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya UVIKO 19. 


Picha 7;Diwani wa Kata ya Uruwira Mh.Yusuph Mlela nae alipata wasaa wa kutoa salamu za Shukrani kwa Rais Samia mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh,Mwanamvua Mrindoko katika Ziara hiyo.

Picha 8;Muonekano wa Vyumba viwili vya Madarasa Lot 1  vilivyokamilika kwa Fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.Shilingi Mil 80 zilielekezwa Uruwira kwa ajili ya Ujenzi.

Picha 9;Muonekano wa Vyumba viwili vya Madarasa Lot 2  vilivyokamilika kwa Fedha za UVIKO 19 katika Shule ya Sekondari Uruwira.Shilingi Mil 80 zilielekezwa Uruwira kwa ajili ya Ujenzi.


Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU February 25, 2025
  • MICHORO YA RAMANI KWA ZABUNI ZILIZOTANGAZWA KATIKA SHULE MBALIMBALI September 16, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 20, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 01, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAMIA DAY: KATAVI YAANDAA TAMASHA KUBWA KUADHIMISHA MIAKA MITANO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    July 02, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI BORA WA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE (LAAC)

    June 19, 2025
  • MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA WAZINDULIWA RASMI NSIMBO, MKOANI KATAVI

    June 09, 2025
  • KAMPENI YA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO

    June 01, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Quick Links

  • Mfumo wa Tausi Portal
  • Watumishi Portal
  • Wezesha Portal
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa PLANREP
  • Mfumo wa SIS
  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa