• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Mazingira na udhibiti wa taka ngumu

 

 

Utangulizi

 

Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, ilianzishwa baada ya kuongezwa kwenye Muundo wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa tangu 29 Januari 2014 ambapo hapo awali ilikuwa ni sehemu ya Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.            


Jina:Vicent Fabian Kasukumpa

Cheo:Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti taka ngumu

Elimu:Shahada ya Mipango ya Mazingira

Taasisi:IRDP-Dodoma

Mawasiliano:Simu: 0756865353    



  •   

    


Jina:Daud B.Buyagu

Cheo:Afisa Mazingira

Elimu: PGDE, OUT - 2012;  BA.GES,UDSM-2009


Mawasiliano:

Simu: +25575686535

+255623355994

Barua pepe:buyagudaud@gmail.com



 

 

   

Majukumu ya Idara

  

Majukumu ya Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu katika  Halmashauri ya Wilaya ya Nsimboyamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni Hifadhi ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu.

 

Sehemu ya kwanza


Hifadhi ya mazingira


  
  • Katika sehemu ya kwanza ya Idara ambayo ni uhifadhi wa mazingira na Bioanuai (Environmental Conservation and Biodiversity) Idara inatekeleza majukumu kama ifuatavyo;
  
  •  Kutenga maeneo ya upandaji miti, majani, maua, ukatiaji miti na upendezeshaji mazingira (Planting of trees, plants, grass, flowers, pruning of trees and beautification) na kusimamia kampeni ya taifa ya upandaji miti.
  
  •  Kuhamasisha jamii kushiriki na kuratibu upandaji miti, majani, maua, ukatiaji miti na upendezeshaji mazingira pamoja na utekelezaji wa mashindano ya Tuzo ya Rais ya kuhifadhi vyanzo vya maji, kupanda na kutunza miti katika Halmashauri husika.
  
  • Kuhamasisha jamii kupanda miti, majani na maua, kukatia majani na miti na kuendezesha Miji na maeneo mbalimbali
  
  • Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya Halmashauri ya usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia mpangokazi wa taifa wa hifadhi na usimamizi wa mazingira.
  
  • Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo na miongozo ya kulinda mazingira ikiwa ni pamoja na bioanuai ardhi, mazingira ya mito, maziwa, bahari na mabwawa.
  
  • K#uweka mfumo wa kukusanya taarifa za mazingira utakao husisha ngazi ya Halmashauri hadi kitongoji/mtaa.
  
  •  Kubaini maeneo ya hatari yanayohitaji usimamizi maalumu na kumshauri waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa mazingira kuhusu njia bora zinazoweza kutumika.
  
  • kuandaa taarifa ya hali ya Mazingira ya maeneo ya Halmashauri zitakazojumuishwa katika ripoti ya taifa yahali yamazingira.
  
  • Kupendekeza maeneo yanayoweza kutangazwa kuwa maeneo ya hifadhi ya taifa ya mazingira na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira ya hifadhi.
  
  • Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari katika maeneo ya mito, maziwa, bahari na mabwawa.
  
  • Kusimamia na kutekeleza sera ya taifa ya mazingira, sheria ya usimamizi wa mazingira kuhusu masuala ya hifadhi ya bioanuai yaliyobainishwa katika sera,sheria, kanuni, miongozo, Mikakati,mipango na programu za kisekta.
 
  • Kutekeleza mikakati, mipango na programu ya mikataba ya kimataifa na kanda inayohusiana na hifadhi ya bioanuai.
 
  • Kuandaa na kutekeleza program za kutoa elimu kuhusu hifadhi endelevu ya bioanuai katika maeneo ya Halmashauri.
 
  • Kubaini bioanuai zilizopo katika Halmashuri na hali ya uharibifu na uhifadhi wake.
 
  • Kuweka na kusimamia mikakati ya kuongoa ardhi iliyoharibiwa na kuzuia uharibifu wa bioanuai.
 
  • Kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya Halmashauri husika.
 
  •  Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na program za Halmashauri kwa kuzingatia Mkakati wa Kitaifa wa Kuhifadhi Bioanuai.
 
  •  Kutekeleza mfumo wa upashanaji habari juu ya Bioanuai na matumizi salama ya Bioteknolojia yakisasa.
 
  • Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala pamoja na majiko bunifu.
 
  • Kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali kuhusu usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira
 
  •  Kutoa mapendekezo na kufuatilia hatua za kukabiliana na uharibifu wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (kama uchimbaji madini, kilimo, ujenzi, ufugaji).
 
  • Kusimamia na kutekeleza kazi nyingine zitakazoelekezwa na Mamlaka za juu
 
  •  
 

B:        Udhibiti na Uchafuzi wa Mazingira (Ardhi, Maji, Hewa na Sauti) (pollution Control: Land, Water, Air and Sound) 

 
  •  Kuandaa na kutekeleza program za kutoa elimu ya mazingira kwa jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa mazingira na athari zake.
  • Kuweka na kusimamia amri za kudhibiti/kuzuia kelele, mitetemo na uchafuzi wa hewa unaosababishwa na moshi, gesitaka au gesi za sumu, kutoka vyanzo mbalimbali kama vile makazi, viwanda, uchimaji wa madini na vyombo vya usafiri.
  • Kuweka miongozo ya kupunguza athari za uchafuzi wa hewa ya ndani ya makazi (in-door pollution) inayosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya nishati ya kuni, vinyesi vya mifugo na uchomaji wa madini ya zebaki.
  • Kuandaa na kusimamia miongozo ya kutenganisha maeneo ya makazi ya watu, ofisi na taasisi za elimu na shughuli za kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanda, madampo ili kudhibiti athari kwa afya na mazingira.
  • Kuandaa miongozo ya ujenzi wa miundombinu ya taka katika maeneo ya biashara, viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi na ya usimamizi wake ili kuhakikisha hali ya usafi na kudhibiti viumbe waharibifu na uzagaaji wa taka.
  • Kuweka na kusimamia miongozo ya usimamizi wa majitaka katika miundombinu ya kuhifadhi kusafirisha na kutibu majitaka kwa kushirikiana na Mamlaka husika.
  • Kufuatilia uzingatiaji wa viwango vilivyowekwa vya majitaka yanayomwagwa kwenye mazingira ili kukidhi viwango vya mazingira.
  • Kusimamia uzingatiaji na utekelezaji  wa viwango vya mazingira vya taifa na kuweka vigezo vya kupima uharibifu wa mazingira.
  • Kufuatilia na kutathmini athari za uchafuzi wa mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji.
  • Kusimamia na kutekeleza sera ya taifa ya mazingira, sheria ya usimamizi wa mazingira kuhusu masuala ya tathmini ya athari kwa mazingira na tathmini ya kimkakati yaliyobainishwa katika sera, sheria, kanuni, miongozo, mikakati, mipango na programu za kisekta.
  • Kufuatilia na kutathmini athari za uchafuzi wa mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji.
  • C:         Tathmini ya athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment)
 

Kuandaa tathmini ya kimkakati kwa mazingira kwa mipango na program za Halmashauri zinazotakiwa kufanyiwa tathmini hiyo kama zilizyobainishwa katika sheria yausimamizi wa Mazingira na kanuni zake

  
  • Kufuatilia utekelezaji wa utaratibu wa Tathmini ya kimkakati ya mazingira katika maeneo ya Halmashauri na kutoa ushauri kwa Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
  • Kufuatilia utekelezaji wa utaratibu wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) katika maeneo ya Halmashauri kwa shughuli zinazotakiwa kufanyiwa (TAM) kama zilizyobainishwa katika sheria ya usimamizi wa mazingira na kanuni zake.
  • Kufuatilia utekelezaji wa Mpango na Masharti ya (TAM) kwa kila shughuli/mradi uliofanyiwa tathmini hiyo au kukaguliwa na kutoa ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
  • Kushirikisha umma katika maamuzi yanayoweza kuathiri mazingira na katika uandaaji wa Sera, Mikakati, Mipango, Programu na Sheria zinazohudu mazingira katika maeneo yao.
  • Kufanya utafiti/uchunguzi wa uharibifu au athari kwa mazingira unaosababishwa na shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo ya Halmashauri na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
  • Kufuatilia na kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizoendelevu kama vile uchimaji madini holela, uvuvi haramu, kilimo kisicho kuwa endelevu, ujenzi holela, ufugaji wa kuhamahama usiozingatia uwezo wa malisho.
  • Kusimamia/kuratibu utekelezaji wa kazi za Kamati za Mazingira na Kamati za Kudumu za Halmashauri.
    

D:        Uhifadhi wa muda, Uchambuzi na Usafirishaji Taka Ngumu (Solid Waste Storage, Sorting, Transportation)

 
  • Kuweka na kusimamia miongozo ya usimamizi wa taka ngumu katika miundombinu ya kuhifadhi, kusafirisha, kuteketeza na kutupa taka ngumu kwa kushirikiana na Mamlaka husika.
  • Kuandaa na kusimamia miongozo ya kutenga maeneo kwa ajili ya kukusanya taka kwa muda ili kuhakikisha kuwa yana ukubwa wa kutosha na kudhibiti athari kwa jamii, Afya na mazingira.
  • Kutenga maeneo maalumu ya kuanzisha vituo vya kukusanya, kuchakata na kuhifadhi taka zitokanazo na vifaa vya umeme na elektroniki, mafuta machafu na taka nyingine za sumu.
  • Kutoa amri inayowataka wenye viwanda na maeneo ya biashara kutenga maeneo ya kutosha, kuweka vifaa vya kutenganisha na kuhifadhi taka, mitambo ya kurejeleza na kurudufu taka ngumu.
  • Kuweka vyombo vya kuhifadhi taka katika maeneo yote ya umma na kuhakikisha usafi wa maeneo hayo.
  •  
 

E:         Uchambuaji, utupaji taka ngumu na uendeshaji Dampo la kisasa (Sorting and Sanitary Disposal of Solid Waste and Dumpsite Management): 

  
  • Kuainisha na kutenga maeneo maalum na ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa dampo za kisasa.
  • Kuweka na kusimamia miongozo ya utupaji wa mwisho wa taka ngumu na uendeshaji wa dampo za kisasa.
  • Kuweka tozo ya usimamizi wa taka inayozingatia gharama halisi ya huduma katika ukusanyaji hadi utupaji katika madampo ya kisasa
 

 

 

Sehemu ya pili:  Udhibiti taka ngumu

 

 

 

Usafirishaji na Ukusanyaji wa Taka Ngumu kutoka kwenye majengo, maeneo ya wazi, barabara na Mifereji ya kuondoa maji ya mvua (Cleaning of Buildings, Open Spaces, Roads na Drainages):

 
  •  Kuweka mifumo na miundombinu isiyoathiri afya na mazingira ya usimamizi wa taka kuanzia zinapozalishwa hadi zinapotupwa kwa kuzingatia utenganishaji, ukusanyaji na uhifadhi, urejelezaji, utekelezaji katika matanuru maalumu na utupaji katika madampo ya kisasa.
  • Kubuni mbinu za kupunguza taka na kusimamia utekelezaji wake ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.
  • Kufanya tafiti/uchunguzi ili kubaini aina ya taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makazi, maeneo ya biashara na taasisi na kubuni njia bora za kupunguza, kutenganisha, kuhifadhi na kutupa taka.
  • Kusimamia usafi katika mifereji ya kukusanya maji ya mvua na kuhakikisha inafanya kazi muda wote.
  • Majukumu yote ya Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu yanatekelezwa kwa kuzingata Sheria Kanuni  na Taratibu zilizopo ndani ya Halmashauri,pamoja na miongozo mbalimbali inayotolewa na Mamlaka za Juu serikalini zinazohusu Utunzani wa Mazingira na Udhibiti Taka Ngumu.
 


Matangazo

  • MAFUNZO YA SENSA KWA WALIOCHAGULIWA KWENYE KAZI YA MUDA YA TEHAMA, UKARANI NA USIMAMIZI WA SENSA July 28, 2022
  • ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KWENYE KAZI YA MUDA YA UKARANI NA USIMAMIZI WA SENSA July 28, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 26, 2022
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO,SHULE YA SEKONDARI NSIMBO MWAKA WA MASOMO 2022/2023 April 08, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • UZINDUZI WA KAMPENI YA UPANDAJI MITI 1,500,000 KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO

    January 25, 2023
  • MILIONI MIA MOJA NA TISA ZATOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

    June 29, 2022
  • Kamati za Sensa za Vitongoji, Vijiji na Kata Nsimbo wajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao

    May 27, 2022
  • DED awashukia Watendaji Nsimbo, Awataka kuacha Visingizio,kukamiilisha miradi ndani ya muda uliopangwa.

    April 21, 2022
  • Angalia zote

Video

ZIara ya Naibu Waziri OR TAMISEMI Mh.David Silinde kukagua Ujenzi wa Madarasa Nsimbo DC
Video zaidi

Quick Links

  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa
  • Orodha ya waheshimiwa madiwani
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Video mbalimbali
  • Muundo wa Halmashauri
  • Picha mbalimbali
  • Fomu mbalimbali

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : 025 295 5164

    Simu: 025 295 5164

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa