Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Kuanzishwa:
Halmashauriya Wilaya ya Nsimbo ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria namba 7 ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2002, Kifungu namba 8 na 9 na kutangazwa kupitia Tangazo la Serikali namba 361 Tarehe 23 Disemba 2012 na kuanza rasmi Julai 1,2013.
Halmashauri hii imeanzishwa kutokana na Halmashauri mama ya Wilaya ya Mpanda iliyokuwa Mkoani Rukwa hapo awali ambapo baada ya kutenganishwa ndipo zilizaliwa Halmashauri za Nsimbo na Mlele.
Mahali ilipo:
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inapakana na Halmashauri 3.Kwa upande wa Kaskazini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Urambo iliyoko Mkoani Tabora,Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ,kwa Upande wa Magharibi inapakana na Manispaa ya Mpanda,kwa Upande wa kusini Nsimbo inapakana na Wilaya ya Sumbawanga iliyoko Mkoani Rukwa,ambapo kwa upande wa Mashariki na Kusini Mashariki inapakana na Wilaya ya Mlele.
Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo yapo katika Kata ya Mtapenda iliyoko njia ya kuwenda Tabora,Kilomita 17 kutoka Mpanda Mjini.
Katika Mipaka ya Kimataifa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inpatikana katika Latitude 5o 0, na 7o 30,kusini mwa Ikweta na Longitudo 29o 0, na 30 o 0,mashariki mwa Griniwichi.
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo inakadiriwa kuwa na ukubwa wa Kilometa za Mraba 14,623,ambayo ni asilimia 30.8 ya eneo lote la Mkoa wa Katavi ambalo ni tambarale yenye miinuko na mabonde machache ambapo karibia eneo lote linatumika kwa shughuli za kibinadamu.
Hali ya Hewa.
Hali ya Hewa ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo hubadilika kutegemeana na mwinuko kutoka usawa wa bahari na hutgemea uoto wa asili wa Vichaka na uoto wa Misitu.
Viongozi wa Halmashauri:
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo tangu kuanzishwa kwake imewahi kuongozwa na Viongozi mbalmbali.Wafuatao ni Wakurugenzi waliowahi kuiongoza Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Rashid Neneka
-Mkurugenzi Mtendaji na Mwasisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo:2013-2015
Michael F.Nzungu
Mkurugnzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
2015-2016
Mwailwa Pangani
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
2017-2018
Mohamed Ramadhani
Mkurugenzi Mtedaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
2018-hadi 2024
Eng. Stephano B. Kaliwa
Mkurugenzi Mtedaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
2024-hadi sasa
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa