• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Nsimbo District Council
Nsimbo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Habari ,Mawasiliano,TEHAMA na uhusiano
      • ununuzi na ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango,Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji na Udhibiti wa maji taka
      • Kilimo,umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma zetu
    • Elimu Msingi
  • Madiwani
    • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shuguli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
    • Jarida Mtandao la wiki la Halmashauri

Elimu Msingi

IDARA YA ELIMU MSINGI

Idara ya Elimu Msingi inatekeleza majukumu mbali mbali kama vile kuandaa, kusimamia, kuratibu na kufuatilia utolewaji wa elimu ya awali, elimu msingi, elimu ya watu wazima, Elimu Maalum na kukusanya takwimu za elimu katika halimashauri kwa kuzingatia Sera na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi.

Wataalamu wa Idara.

 

Jina: Marcus K. Nazi

Cheo: Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi.

Elimu:Shahada ya Kwanza ya  Sanaa katika ELimu

(Chuo Kikuu Teofilo Kisanji  TEKU-Mbeya)

Mawasliano: 

Simu-+255756444455 au +255782311926

Email:nazirimarcus@gmail.com

 

Jina:Edwin J. Fande

Cheo: Afisa Taaluma Wilaya Msingi

Elimu:Stashahada ya Elimu.

(Chuo Cha Ualimu Butimba)

Mawasiliano:

 Tel: +255756843456

Email: Edwinfande2015@gmail.com

 

 

Jina: Clever M. Mngao

Cheo: Afisaelimu Elimu Maalum Wilaya

Elimu: Shahada ya Kwanza ya Elimu- Elimu Maalum

(Chuo Kikuu Cha Tumaini SEKUCO-Tanga)

Mawasiliano:

 Tel: +255762393027

Email: cmngao@yahoo.com

 

Jina: Jackson Aloyce

Cheo: Afisa elimu Vifaa na Takwimu Wilaya.

Elimu:Shahada ya Kwanza ya  Sanaa katika ELimu

(Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustine Tanzania RUCO-Iringa)

Mawasliano: 

Simu-+255755999439

Email:jacksonaloyce35@gmail.com

 

 

Jina: Josephat J. Mchayano

Cheo: Afisa elimu Msaidizi Vifaa na Takwimu Wilaya.

Elimu: :Shahada ya Kwanza ya  Sanaa katika ELimu

(Chuo Kikuu Teofilo Kisanji TEKU-Mbeya)

                                                                                           Mawasliano: 

Simu-+255757452943

Email:mchayanojj@gmail.com

 

 

Jina: Oliver Joseph

Cheo: Kaimu Afisa Elimu ya Watu Wazima.

Elimu: :Shahada ya Kwanza ya  Sanaa katika ELimu

(Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania)

                                                                                           Mawasliano: 

Simu-+255628978762

Email:oliverjoseph94@yahoo.com

 

 

Jina: Didas Benard Mwanahewa

Cheo: Afisa elimu Msaidizi Taaluma.

Elimu: :Shahada ya Kwanza ya  Sanaa katika ELimu

(Chuo Kikuu Teofilo Kisanji TEKU-Mbeya)

                                                                                           Mawasliano: 

Simu-+255753478072

Email:mwanahewad2003@gmail.com

 

 

 

Jina: Zurieth Chubwa

Cheo: Katibu Mahsusi daraja I.

Elimu:Certificate in Secretarial Services

Chuo:Chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora

                                                                                           Mawasliano: 

Simu-+255762286961

 

Jina: Vaileth  Lubendegele

Cheo:  Mtunza Kumbu Kumbu.

Elimu:Certificate in Record Management

Chuo:Chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora

                                                                                           Mawasliano: 

                  Simu-+255763848287

              Email:mailaclarissa@gmail.com




MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI

  1. Upanuzi na uimarishaji wa Elimu Msingi
  2. Kuendesha mafunzo ya utunzaji na usimamizi wa fedha kwa kamati za shule, walimu na wanafunzi.
  3. Kusimamia wajibu, haki au maslahi ya walimu
  4. Kukusanya takwimu za shule za Msingi na kuzihifadhi, kuzitumia na kutuma kule zinakohitajika, mfano Ofisi ya RAIS TAMISEMI, WEST nk.
  5. Kufanya maandalizi kwa ajili ya watahiniwa wa Madarasa yanayofanya mitihani ya kitaifa na kuratibu mitihani yote ya Kitaifa kwa Shule za Msingi.
  6. Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa shule ya msingi.
  7. Kufuatilia uhai wa kamati za shule na ununuzi wa vifaa vya shule.
  8. Kusimamia mafunzo ya walimu kazini katika ngazi zote; Astashahada, Stashahada na Shahada.
  9. Kuratibu na kusimamia mpango wa EWW, MUKEJA na MEMKWA
  10. Kuhakikisha kuwa fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya shule yaani, Capitation Grant na Development Grant zinapelekwa shuleni kwa wakati na kufuatilia matumizi ya fedha hizo.
  11. Kutekeleza maagizo mbali mbali kutoka ngazi za juu kwa wakati.
  12. Kufanya tathmini ya mitihani mbalimbali inayofanyika,mfano; ya kiwilaya, kimkoa na kitaifa ili kubaini mafanikio na mapungufu ya Mtaala na kuchukua hatua pale inapogundulika kuwa kuna udhaifu.
  13. Kusimamia na kufuatilia masuala yote ya mtambuka
  14. Kusimamia na kuratibu zoezi zima la michezo shuleni.

KAZI NA MAJUKUMU YA KILA MTUMISHI

(i)  AFISA ELIMU

      Afisaelimu wa Wilaya ana majukumu yafuatayo: -

  1. Kusimamia majukumu yote ya Idara na ya kila mtumishi katika Idara
  2. Kupanga, kuratibu na kusimamia masuala yote ya Idara ya Elimu katika Wilaya.
  3. Kupanua na kuimarisha Elimu Msingi
  4. Kusimamia wajibu na maslahi ya watumishi katika Idara ya Elimu
  5. Kukagua na kufuatilia taarifa za ukaguzi wa Elimu Msingi
  6. Kuandaa na kusimamia uendeshaji wa mitihani ya Elimu ya Msingi hasa darasa la IV na VII ya Taifa kila mwaka.
  7. Kusimamia mgao na mipango ya fedha kwa ajili ya uendeshaji wa masuala ya kielimu.
  8. Kuwaendeleza walimu kitaaluma na kitaalamu ili watoe huduma bora zinazokidhi viwango vya WEST.
  9. Kutekeleza maagizo mbalimbali kutoka ngazi za juu kwa wakati.

    (ii) AFISA ELIMU TAALUMA

Afisaelimu Taaluma wa Wilaya ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kupanga, kuratibu na kusimamia taaluma katika Wilaya.
  2. Kufuatilia ufundishaji katika shule za msingi na kusimamia Mtaala wa Elimu.
  3. Kukusanya takwimu za watahiniwa wa darasa la IV na VII kutoka shuleni kuzihakiki na kuziwasilisha Mkoani kila mwaka.
  4. Kufuatilia taarifa za ukaguzi wa elimu ya msingi.
  5. Kufuatilia na kutoa ushauri kwa walimu juu ya utekelezaji wa mitaala ya elimu na mihtasari.
  6. Kupanga, kuratibu na kusimamia uendeshaji wa mitihani ya darasa la IV na VII ya Wilaya, Mkoa na Taifa kila mwaka.
  7. Kutathimini mitihani ya darasa la IV na VII ili kubaini mafanikio na udhaifu na kurekebisha mapungufu.
  8. Kupanga na kuendesha semina kwa Walimu Wakuu, Walimu Wakuu Wasaidizi na Waratibu Elimu Kata.
  9. Kufuatilia utoro wa walimu katika vituo vya kazi.
  10. Kuanzisha na kuhimiza matumizi bora ya vituo vya walimu TRC
  11. Kutekeleza maagizo yote kutoka ngazi za juu.

      (iii) MAJUKUMU YA AFISAELIMU WA VIFAA NA TAKWIMU WA WILAYA 

  1. Kusimamia Upanuzi na uimarishaji wa Elimu Msingi.
  2. Kusimamia na kufuatilia uanzishaji wa shule mpya
  3. Ukusanyaji – uhifadhi na utoaji wa takwimu za elimu ya msingi yaani kupokea, kuzichanganua, kuzifafanua na kuziwasilisha zinakotakiwa bila kuchelewa.
  4. Kujua idadi ya Mahitaji ya walimu, kufanya makisio ya idadi, kwa madaraja, kufuatana na upungufu na upanuzi.
  5. Vifaa vya shule – uagizaji na usambazaji kufuatana na mahitaji ya shule na fungu la fedha.
  6. Mitihani – usimamizi, usafirishaji na usalama wake.
  7. Fedha – usimamizi, yalingane ya mahitaji.
  8. Huduma kwa wanafunzi – mahudhurio, uhamisho, chakula cha mchana.
  9. Kufanya kazi zingine atakazopewa na Afisaelimu wa Wilaya.

     (iv) AFISA ELIMU YA WATU WAZIMA

    Afisa elimu ya Watu Wazima anatakiwa kuwa na majukumu yafuatayo:-

  1. Kupokea, kuhifadhi na kusambaza vifaa vya EWW
  2. Kuandaa na kutunza kumbukumbu zote za EWW
  3. Kutathmini mipango mbalimbali ya EWW katika Wilaya
  4. Kusimamia taaluma ya uandishi wa vitabu vya kiada na ziada na rejea mbalimbali.
  5. Kusimamia uanzishaji na uendeshaji wa maktaba za kata na vijiji.
  6. Kushirikiana na Afisa elimu Taaluma kuandaa vielelezo mbalimbali vya kuboresha ufundishaji
  7. Kuandaa na kuendesha mafunzo kwa njia ya filamu, video, runinga, mabango na vipeperushi.
  8. Kushirikiana na Afisaelimu Taaluma wa Sekondari kuandaa vielelezo mbalimbali ili kuboresha ufundishaji
  9. Kushirikiana na Mkutubu wa Mkoa, Afisaelimu Taaluma Msingi na Sekondari kuanzisha na kusimamia Maktaba za Kata, vijiji, Shule za Msingi na Sekondari.
  10. Kufanya kazi mbalimbali kutoka ngaza za juu.

 (v) AFISA ELIMU UFUNDI

Kama Afisaelimu Ufundi ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kuratibu na kusimamia Elimu ya Ufundi katika shule za msingi, sekondari na vituo vya EWW.
  2. Kumshauri Afisaelimu (W) Msingi, Sekondari na EWW kuhusu masuala ya Elimu ya Ufundi
  3. Kushirikiana na Afisa elimu Vifaa na Takwimu, kusimamia ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, vyoo na kutengeneza samani za shule
  4. Kushirikiana na Mhandisi wa Wilaya kuhusu miundombinu mbalimbali ya shule.
  5. Kuhamisha walimu wenye taaluma ya ufundi kujiunga na mafunzo ya ufundi ili kupata walimu wataalamu.
  6. Kuandaa na kuendesha warsha juu ya elimu ya ufundi kwa walimu
  7. Kufanya kazi zote atakazopewa kutoka ngazi za juu .

(vi) AFISA ELIMU WA ELIMU MAALUM

Afisa Elimu Maalumu anahusika kufanya yafuatayo katika ngazi ya Wilaya:-

  1. Kuandaa bajeti ya Elimu Maalum katika Wilaya ili kufuatilia mahitaji ya shule au vitengo ngazi ya Wilaya.
  2. Kutunza kumbukumbu za walimu wataalamu na wale wenye ulemavu kwa kuzingatia jinsi, umri na aina ya ulemavu.
  3. Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa elimu maalumu ya kila robo mwaka na kuziwasilisha panapo husika.
  4. Kushirikiana na sekta za Afya, Maendeleo ya Jamii, Mashirika binafsi na Umma kuendeleza elimu maalumu kwa shule za msingi na sekondari.
  5. Kushirikiana na Afisaelimu Vifaa na Takwimu, Afisaelimu Ufundi na Mhandisi juu ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, vyoo na mahitaji ya wenye ulemavu.
  6. Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya utoaji wa elimu katika shule
  7. Kutunza kumbukumbu za vifaa vya kufundishia na kujifunzia
  8. Kufanya kazi mbalimbali kutoka ngazi za juu.

     (vii) AFISA ELIMU SAYANSI KIMU

    Afisaelimu Sayansi Kimu  na Afya wa Wilaya ana majukumu

    yafuatayo:-

  1. Mshauri wa Afisaelimu Msingi, Sekondari na Elimu ya Watu Wazima kuhusu masuala ya elimu ya Sayansi Kimu na Afya katika Halmashauri.
  2. Kusimamia elimu ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi
  3. Kuratibu shughuli zote za afya na lishe katika shule za msingi, sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.
  4. Kuandaa makadirio ya matumizi ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari na vituo vya EWW nje ya mfumo rasmi ili yaingizwe katika  mipango na bajeti za Halmashauri.
  5. Kushirikiana na Afisaelimu Taaluma Msingi na Sekondari kutoa ushauri na kuandaa mafunzo kwa walimu wanaofundisha somo la sayansi kimu na afya katika shule za msingi, sekondari na vituo vya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.
  6. Kutoa ushauri nasaha na unahisi kwa walimu, wazazi na wanafunzi kuhusu afya ya uzazi, malezi bora na tabia njema.
  7. Kuanzisha vituo vipya vya sayansi kimu na afya katika shule za msingi na sekondari na kushauri namna ya kuviendesha kufuatana na mwongozo wa Wizara.
  8. Kutafuta na kusimamia usambazaji wa vifaa vyote vya sayansi kimu na afya katika shule.
  9. Kutayarisha taarifa za utekelezaji wa elimu ya sayansi kimu na afya ya kila robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha katika sehemu zote zinazohusika.
  10. Kushirikiana na watendaji wa sekta ya afya, maji, maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii pamoja na mashirika ya kijamii katika kuendeleza elimu ya sayansi kimu na afya katika shule za msingi na sekondari.
  11. Kuhamasisha wenye taaluma ya sayansi kimu na afya kujiunga na mafunzo ya elimu ya sayansi kimu na afya kwa lengo la kupata walimu wataalamu.
  12. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

    (viii) AFISA MICHEZO NA UTAMADUNI

Afisaelimu Michezo na Utamaduni ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kupanga, kuratibu na kusimamia michezo katika shule za msingi.
  2. Kusimamia sera za michezo na utamaduni wa Kitanzania katika shule za msingi.
  3. Kumshauri Afisa elimu wa Wilaya kuhusu masuala ya michezo na utamaduni.
  4. Kuratibu mashindano ya michezo katika shule za msingi ngazi ya Wilaya
  5. Kupanga bajeti ya vifaa vya michezo katika shule za msingi.
  6. Kusimamia matumizi sahihi ya fedha zinazokasimiwa kwa shughuli za michezo.
  7. Kusimamia elimu, michezo na utamaduni kwa shule za msingi ngazi ya Wilaya.
  8. Kuhamasisha upatikanaji wa walimu wa michezo shuleni.
  9. Kufanya kazi mbalimbali anazopangiwa na Mkuu wa Idara na kutoka ngazi za juu n.k.

    (ix)  BOHARIA

Boharia wa Idara ya Elimu ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kuagiza, kupokea vifaa vya Idara ya Elimu Msingi na Sekondari
  2. Kutunza vifaa vyote vya Idara ya Elimu
  3. Kuratibu na kufanya manunuzi ya vifaa vya elimu
  4. Kuhakikisha usalama wa vifaa vya Idara ya Elimu
  5. Kugawa vifaa mbalimbali vya elimu katika shule za msingi
  6. Kutoa vifaa na mafuta kwa ajili ya madereva katika Idara
  7. Kusimamia uhamishwaji wa walimu kutokea kituo kimoja hadi kingine
  8. Kutoa semina kwa walimu juu ya ununuzi na utunzaji wa vifaa vya Umma
  9. Kufanya kazi zote kutoka kwa viongozi wake
  10. Kutunza nyaraka zote za manunuzi.

(x)   WATUMISHI WASIO WALIMU

(xi)  OS

Kama Msaidizi wa Ofisi ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kuwahi kufungua milango ya ofisi kila siku ya kazi
  2. Kufanya usafi wa ofisi na vifaa vya ofisi kila siku
  3. Kutunza kumbukumbu za watumishi wa Idara kila siku
  4. Kutunza na kuhakikisha usalama wa majalada
  5. Kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kwa wakati
  6. Kufanya kazi zote anazoagizwa na Mkuu wake wa kazi.

    (xii)  WAHUDUMU WA MASIJALA.

  Msaidizi wa Ofisi ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kuwahi kufungua milango ya ofisi kila siku ya kazi
  2. Kufanya usafi wa ofisi na vifaa vya ofisi kila siku
  3. Kutunza kumbukumbu za watumishi wa Idara kila siku
  4. Kutunza na kuhakikisha usalama wa majalada
  5. Kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kwa wakati
  6. Kufanya kazi zote anazoagizwa na Mkuu wake wa kazi.

    (xiii)  MHASIBU WA IDARA.

Kama bwana fedha wa Idara anawajibika:-

  1. Kuandika vocha
  2. Kuandika hundi
  3. Kuandaa taarifa ya mapato na matumizi
  4. Kuandaa masuluhisho ya benki (Bank Reconciliation)
  5. Kuandaa taarifa ya robo mwaka PEDP (QUARTERLY REPORT)
  6. Kulipa posho watumishi wa Idara
  7. Kufanya kazi mbalimbali kutoka ngaza za juu.

    (xiv) KATIBU MUHTASI WA IDARA.                                                                                                                                             

Kama Katibu Muhtasi wa Afisaelimu ana majukumu yafuatayo:-

  1. Kupokea simu za ofisi
  2. Kupokea wageni na kuwaelekeza
  3. Kuchapa nyaraka mbalimbali za ofisi
  4. Kufanya usafi katika ofisi yake
  5. Kutunza majalada ya siri (Confidential files)
  6. Kupokea na kupeleka majalada ya siri
  7. Kudurufu nyaraka mbalimbali za ofisi
  8. Kufanya kazi mbalimbali kutoka kwa Msimamizi wa kazi katika Idara.

 

 

 

 

Matangazo

  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO,SHULE YA SEKONDARI NSIMBO MWAKA WA MASOMO 2022/2023 April 08, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • DED awashukia Watendaji Nsimbo, Awataka kuacha Visingizio,kukamiilisha miradi ndani ya muda uliopangwa.

    April 21, 2022
  • Mwenyekiti Nsimbo awataka Watendaji kukamilisha Malengo kuelekea Mwishoni mwa Mwaka wa Fedha

    April 21, 2022
  • ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA KUFANYA KAZI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO

    March 23, 2022
  • Kaimu DED Nsimbo akagua Ujenzi Miradi Kata ya Ugalla, Asisitiza maandalizi ya manunuzi ya Vifaa kwa wakati kutoathiri kasi ya Ujenzi.

    March 22, 2022
  • Angalia zote

Video

ZIara ya Naibu Waziri OR TAMISEMI Mh.David Silinde kukagua Ujenzi wa Madarasa Nsimbo DC
Video zaidi

Quick Links

  • Kupata matokeo ya kidato cha nne ingia hapa
  • Orodha ya waheshimiwa madiwani
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Video mbalimbali
  • Muundo wa Halmashauri
  • Picha mbalimbali
  • Fomu mbalimbali

Kurasa zinazohusana

  • President's Office
  • Tanzania Government Portal
  • Public service Management
  • Public Service Recruitment
  • PO- RALG

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    Mpanda to Tabora road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda

    Simu : +255739992124

    Simu: +255787992124

    Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Malalamiko
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa