WASIFU WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
Idara ya Elimu Sekondari ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ina jukumu kubwa la usimamizi uratibu, ufuatiliaji, pamoja na uandaaji wa Mipango na mikakati ya uendeshaji wa Shule zote za Sekondari, walimu, wanafunzi na watumishi wengine katika idara. Idara pia inalo jukumu la kuandaa bajeti na mahitaji ya samani, miundombinu pamoja na vifaa vyote vinavyohitajika katika elimu ya Sekondari.
Wataalamu wa Idara
Jina: Said J. Mmaraba
Cheo: Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari
Elimu: Shada ya kwanza ya Sayansi katika Elimu
(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-Dar es Dalaam)
Mawasliano:
Simu-+255759430979
Email: smmaraba@yahoo.com
Jina: Amani Gisbert Ntibakazi
Cheo: Afisaelimu Vifaa na Takwimu
Elimu: Shahada ya kwanza ya Elimu
(Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-Mwanza)
Mawasiliano:
Tel: +255767061789
ntibakazig@gmail.com
Jina: Msambya Sady Ally
Cheo: Mwalimu IIIC
ELimu: Shahada ya kwanza ya Elimu
(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Dar es salaam)
Mawasiliano:
Simu: +255766900847
E-Mail- almsambya@gmail.com
Jina: Mhangwa J. Sekule
Cheo: Mwalimu IIIC
Elimu: Shahada ya Uzamili katika Elimu
(Chuo cha Mtakatifu Yohana-Dodoma)
Mawasiliano:
+255769721411
Majukumu ya Idara:
1. Kuwasilisha taarifa za elimu ya Sekondari katika ngazi zote za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
2. Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya Sekondari.
3. Kusimamia na kudhibiti mapato na matumizi ya elimu ya Sekondari na kuhakikisha kuwa fedha za Elimu ya Sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa ie, kununulia vitabu, vifaa vya kujifunzia na vifaa vya michezo.
4. Kusimamia upanuzi wa elimu ya Sekondari.
5. Kusimamia na kuratibu maslahi ya Walimu na Watumishi wasio Walimu katika ngazi ya Sekondari.
6. Kuratibu na kusimamia mitihani ya Kitaifa inayoendeshwa katika Shule za Sekondari.
7. Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu ya Sekondari ya kila mwaka.
8. Kufuatilia na kutathimini maendeleo ya Elimu ya Sekondari
9. Kuhimiza Shule zote kuboresha miundo mbinu ya kujifunza na kufundishia kama vile ujenzi wa madarasa, maabara, vyoo na nyumba za Walimu.
10. Kuhiniza na kudhibiti nidhamu ya Walimu na Wanafunzi wa Shule za Sekondari.
11. Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo ya Shule za Sekondari katika Harimashauri.
12. Kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya Sekondari.
13. Kuhakikisha kuwa Walimu wote wanaoajiriwa wanapangwa katika Shule kuzingatia ikama.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa