IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ina vitengo vya Uthamini, Mipango Miji, na Urasimu wa Ramani, Upimaji Ardhi, Ardhi Utawala, na Maliasili. Kwa ujumla lengo kuu la Idara ni kuhakikisha maendeleo endelevu ya Wilaya na uhifadhi wa maliasili Mazingira kwa manufaa ya wananchi kwa sasa na vizazi vijavyo. Shughuli zinazofanywa ili kufikia lengo hilo kuu ni pamoja na;
Misitu.
Halmashauri ina hekta 11,552,200ha za Misitu na maeneo ya Uwindaji. Misitu hii ni ya Msaginya,Mpanda North East F.R, Mlele Hills F.R, na Maeneo ya uwindaji ya Mlele kaskazini na msima magharibi iliyopo ugalla.
Shughuli za Kiutalii
Hifadhi ya taifa ya Katavi ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo na Mlele. Hifadhi hii hupokea wageni wa ndani na nje ya nchi kutoka duniani kote. Hifadhi huendesha shughuli za kuongoza watalii, kupiga picha, malazi, kutoa chakula kwa watalii na shughuli zingine muhimu za kiutalii
Uwindaji wa kitalii.
Kwa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, shughuli za uwindaji wa kitalii hufanyi katika vitalu wiwili vya Msaginya West (3,500 km2) na Mulele North Hunting Block (3,000 km2).
Mafanikio
Katika kipindi cha 2015/2016 jumla ya viwanja 2002 vilibuniwa na kati ya hivyo viwanja 576 vimepimwa na taratibu za ugawaji zinaendelea baada ya uthamini kukamilika. Pia jumla ya miti 674,500 imepandwa katika maeneo mbali mbali ya wilaya. Aidha Ili kuhakikisha kasi ya upimaji wa viwanja katika maeneo ya wilaya, idara inatarajia kununua vifaa cha upimaji viwanja “Total station”, “GPS” na “Ranging poies” Vifaa hivi vitasaidia idara kuboresha na kurahisisha utoaji huduma kwa wakazi wa Nsimbo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa