Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mheshimiwa Filbert H. Sanga ameongoza kampeni ya upandaji miti katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo akiwa ni mgeni Rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo katika chanzo cha Mto Ndurumo Kata ya Mtapenda Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Filbert H. Sanga aliongoza zoezi la upandaji miti ambapo jumla ya miche 150 aina ya Mikuyu, ilipandwa katika chanzo cha mto Ndurumo ikiwa ni mkakati wa kuvitunza vyanzo vya maji, pia ikiwa ni mkakati kabambe wa Kitaifa wa kuhakikiksha kila Halmashauri inapanda miche 1,500,000 na kuisimamia kwa ukaribu.
Pamoja na uzinduzi huo katika chanzo cha maji Halmashauri imeweza kupanda miche 6169 katika kata 7 kati ya 12 zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kuanzia tarehe 18/01/2023 mpaka leo tarehe 25/01/2023.
Tarehe 18/01/2023 Halmashauri ilipanda Miti katika Kata ya Sitalike pamoja na Kata ya Nsimbo. Katika Kata ya Nsimbo jumla miti 1,263 ilipandwa ikiwa miti 500 ilipandwa katika Shule ya Sekondari ya Anna Lupembe, miti 600 ilipandwa katika Shule ya Msingi Isanjandugu, Miti 100 katika Shule ya Msingi Tulieni na Miti 63 ilipandwa katika zahanati ya Isanjandugu. Pia katika kata ya Sitalike jumla ya miti 555 ilipandwa ikiwa miti 150 ilipandwa katika Shule ya Msingi Sitalike, 100 Shule ya Msingi Matandalani, 50 Shule ya Msingi Magula, 105 Shule ya Msingi Mtisi na 150 Shule ya Sekondari Sitalike.
Tarehe 19/01/2023 Halmashauri ilipanda Miti 950 katika Kata ya Mtapenda, kati ya miti hiyo miti 150 ilipandwa katika hospitali ya Wilaya ya Nsimbo, miti 300 ilipandwa katika Shule ya sekondari Mtapenda na miti 500 ilipandwa katika Shule ya Msingi Isinde.
Tarehe 20/01/2023 jumla ya miti 2533 ilipandwa katika kata za Itenka, Ibindi, Kapalala na Machimboni ikiwa ni katika Shule za Msingi, Shule za Sekondari, kituo cha Afya Itenka, ofisi za Kata na Makao makuu ya Halmasauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Tarehe 24/01/2023 Miti 150 ilipandwa katika chanzo cha Mtapenda.
Idadi hiyo ya miche ya miti imejumulisha miche ya matunda (mipapai,mipera,matunda damu), Muarobaini, Mikangazi, Mikuyu (miche rafiki na Mazingira), Mijohoro, Jakaranda na Majani mapana (mbao).
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mhe. Halawa Charles Malendeja amewapongeza na kuwashukuru wadau pamoja na taasisi mbalimbali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha malengo ya Upandaji miti kitaifa yanafikiwa katika Halmashauri yetu na Wilaya ya Mpanda kwa ujumla. Wadau pamoja na taasisi hizo ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS wilaya ya Mpanda na Kanda ya Magharibi, Vyama vya Ushirika vya Katumba, Nsimbo na Ivungwe, Taasisi ya Jane Goodall na wananchi wote wa Halmashauri ya Nsimbo kwa ujumla wao na mwitikio wa upandaji miti.
“Tunza Mazingira tuing’arishe Nsimbo”
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa