Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika Jumatano ya Tarehe 29.10.2025, Makarani waongozaji wapiga kura katika vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Nsimbo leo wamepewa mafunzo elekezi katika Jimbo la Nsimbo lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Akifungua mafunzo hayo mapema hii leo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Nsimbo Bwana Julius Z. Moshi amewasihi Makarani hao kuwa makini katika kipindi chote cha mafunzo yanayotolewa na watendaji wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, na hatimaye waweze kufuata taratibu, kanuni, sheria na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. “Ninyi mlioitwa kuja kupewa mafunzo hapa, mnapaswa kufuata taratibu, kanuni, sharia na miongozo na maelekezo yote yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi……..” ameongeza Bwana Moshi.
Bwana Julius Moshi amewasisitiza makarani hao kusoma katiba, sheria na miongozi inayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kupata uelewa zaidi na na kuuliza kwa watu sahihi jambo lolote litakalohitaji ufafanuzi ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi. Bwana Moshi amewataka makarani hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha ufanyaji kazi kazi katika vituo vya kupigia kura. “fanyeni kazi kwa ushirikiano kama timu ili kurahisisha ufanyaji kazi kazi katika vituo vya kupigia kura…..” Amesema Bwana Moshi.
Makarani waongozaji wapiga kura wametakiwa kuzingatia unadhifu na kuwa na lugha ya staha kwa wapiga kura wote watakaofika katika kituo cha kupigia kura. “Hakikisheni mnazingatia unadhifu, lugha nzuri na kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalum wakapofika kituoni”
Aidha, baada ya mafunzo hayo, msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Nsimbo Bwana Julius Moshi amewapongeza wakufunzi pamoja washiriki wote wa mafunzo kwa uvumilivu, utulivu na umakini wao katika kipindi chote cha mafunzo.
Bwana Moshi amewasihi washiriki wa mafunzo kutunza siri katika kipindi chote cha upigaji kura kama ambavyo wamekula kiapo chao cha kutunza siri. Bwana Moshi amesema ukikwaji wa kiapo walichokula ni makossa kwa mujibu wa sheria za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi “washiriki wa mafunzo, kabla ya kuanza mafunzo mliapa kiapo cha kutunza siri, kipao hiki kipo kwa mujibu wa kanuni ya nane ya kanuni za uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani za mwaka 2025……”
Katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku moja, jumla ya makarani 305 walihudhuria na kupewa mafunzo elekezi yatakayowaongoza kutekeleza majukumu yao katika jumla ya vituo 281 vitavyotumika katika upigaji kura katika Jimbo la Nsimbo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa