Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imejidhatiti kikamilifu kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri hiyo kupitia vyanzo mbalimbali vya fedha.
Katika Halmashauri hiyo, Timu ya Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) imeendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri hiyo. Timu hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa idara ya mipango Bwana Mohamed Hussein, pamoja na miradi mingine, imekagua miradi ya afya na elimu.
Katika Kata ya Ugalla, timu hiyo imekagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kalele ambapo ujenzi umefikia katika hatua ya ukamilishaji. Katika hatua hiyo ya ukamilishaji, mradi huo ulitengewa kiasi cha shilingi milioni 35 ambapo tayari vifaa vimefika katika eneo hilo tayari kuanza kazi. Aidha, baadhi ya wazabuni walioshinda tenda ya kupeleka vifaa na bado havijafika katika eneo la mradi wamepewa siku tatu kuhakikisha vifaa vyote vimefika.
Aidha, katika mradi wa ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi katika Kijiji cha Katambike, mradi huo unaendelea na ujenzi uko katika hatua ya kunyanyua kuta kwa baadhi ya majengo. Ujenzi huo unaoendelea uko nyuma ya muda kutokana na uchache wa mafundi katika eneo la mradi. Ambapo mkandarasi ameagizwa kuongeza idadi ya mafundi ili mradi huo uwe umekamilika ifikapo disemba 23 mwaka huu kwa mujibu wa mkataba.
Bwana Mohamed Hussein amemuagiza mhandisi kusimamia vizuri mradi huo ili ukamilike kwa haraka.
“engineer simamia tarehe 23 majengo haya yakamilike, wakupe mpango kazi wa mpaka tarehe 23…”
Katika mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Lukama unaotekelezwa katika Kata ya Litapunga, mradi huo uko katika hatua ya upauaji ambapo tayari kazi ya kuezeka bati imekamilika na mafundi wanaendelea na shughulo zingine za ukamilishaji wa mradi huo.
Mradi wa ujenzi wa Zahanati hiyo ulioanzishwa kwa nguvu za wananchi ulipewa kiasi cha shilingi milioni 65 katika hatua za ukamilishaji wake.
Pamoja na miradi mingine timu hiyo ya ufuatiliaji na Tathmini imesisitiza mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi yote ikamilike kwa wakati.


Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa