Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda ikiongozwa na Mwenyeki wake Ndugu Joseph Aniseth Lwamba, imefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayoendelaea ndani ya Hamlshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Ziara hiyo imefanyika Disemba 19, 2025 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo aliongozana na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mheshimiwa Jamila Yusuph, Mkurugenzi mtendaji wa Halmahsauri ya wilaya ya Nsimbo Bi Christina Bunini, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh. Annah Lupembe pamoja na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Akizuungumza baada ya ukaguzi wa Mradi wa Maji katika kijiji cha Kabuge Mwenyekiti wa kamati hiyo amemtaka mhandisi wa mradi huo kuongeza kasi ya jenzi ya miundo mbinu kwenye chanzo cha Maji ya Mradi huo ili wananchi waweze kufaidika mapema na huduma hiyo.
“Nadhani kuna haja sasa wahandisi wote wahamie huku ili tuone hii hatua ya kwanza kama itaweza kufanikiwa na hatimae wananchi waweze kupata Maji”
Kamati hiyo pia imetembelea mradi wa ujenzi wa Daraja la Ikondamoyo katika kijiji cha Ikondamoyo Halmashauri ya Wilaya Nsimbo, ambao upo kwenye hatua za mwisho za ukamilishaji wake. kamati hiyo kupitia mwenyekiti wake imempongeza Mkandarasi wa Mradi huo kwa kasi na ubunifu aliouonesha wa kufanya ujenzi kwa kutumia mawe hali inayopunguza gharama ya ujenzi na kuongeza ubora kwani miradi mingi inayojengwa kwa namna hiyo hudumu kwa muda mrefu.
Aidha kamati hiyo imekagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo hususani ujenzi wa Jengo la Utawala, jengo la wazazi, jengo la kufulia pamoja na jengo la Bohari ya Dawa, ambapo Halmashauri tayari imepokea jumla ya Tsh Milioni Mia nne (400,000,000) kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo ambayo yapo kwenye hatua za mwisho.
Kiongozi wa Kamati hiyo Ndugu Joseph Lwamba amempongeza Mkuu wa wilaya Mpanda Mh. Jamila Yusuph pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Bi. Christina Bunini kwa kusimamia vizuri mradi huo na kumuagiza mkandarasi kuhakikisha anaharakisha ujenzi wa Majengo hayo ili wanachi waweze kupata huduma zote za msingi za Afya kwenye hospitali hiyo.
Kamati hiyo imekamilisha ziara yake ya ukaguzi wa Miradi, kwa kutembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Ibindi kilichopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya Nsimbo ambapo ujenzi wake upo kwenye hatua ya kusimamisha kuta, na hivyo mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndugu Joseph Aniseth Lwamba amemuagiza mkandarasi wa Mradi huo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema kwani eneo hilo ni makaazi ya watu wengi hivyo kukamilika kwake kutarahisisha upatikakaji wa huduma za Afya kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa