Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mheshimiwa Jamila Yusuph Kimaro, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kusimamia kwa ukaribu mchakato wa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2026, ili kuhakikisha watoto wote wenye sifa wanaanza masomo ifikapo Januari 2026.
Mheshimiwa Jamila ametoa agizo hilo Disemba 10, 2025 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (District Consultative Committee – DCC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi. Ametaka Wakurugenzi hao kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri na sifa za kuanza shule anaandikishwa ndani ya muda uliopangwa.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri hizo kusimamia kikamilifu sheria zinazokataza utumikishwaji wa watoto, huku akisisitiza kufanya ukaguzi katika maeneo ya machimbo ya madini ili kubaini watoto wanaofanya shughuli hizo na kuhakikisha wanarejeshwa shuleni.
Jambo lingine ni kwa Wakurugenzi kufanya ukaguzi kwenye maeneo ya machimbo ya madini kwa lengo la kuwabaini watoto ambao wanatakiwa kuwa shuleni, wakasimamie sheria zinazokataza utumikishwaji wa watoto katika maeneo hayo, alisema.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Afisa Mipango Bw. Alfred John Rukelegwa alisema kuwa hadi kufikia Disemba 2026 jumla ya wanafunzi 3,902 wameandikishwa kuanza elimu ya msingi katika Halmashauri hiyo. Kati yao wasichana ni 1,936 na wavulana 1,966, sawa na asilimia 51ya lengo la uandikishaji.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Jamila amezitaka Halmashauri hizo kufanya mchakato wa kutambua vijana waliopo katika maeneo yao kulingana na elimu, taaluma na shughuli wanazofanya ili kurahisisha serikali kuwafikia na kuwapatia fursa na misaada ya kuwawezesha kiuchumi.
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa