Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi ambapo hekta 2,778,330 za ardhi zinafaa kwa kilimo.
Mazao makuu ya chakula ni mihogo, mahindi, mpunga, viazi vitamu, ndizi, ulezi, viazi mviringo, mboga za majani na matunda.
Mazao makuu ya biashara ni Tumbaku, Karanga, Alizeti, Ufuta na Miwa. Shughuli za uvuvi hufanyika katika mto Ugalla na Katuma.
Katika jumla ya hekta 2,778,330 zinazofaa kwa shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara,ati ya eneo hilo hekta 806 zinafaa kwa shughuli za umwagiliaji katika skimu 4 kubwa ambazo ni skimu ya Ugalla 225Ha, Uruila 350Ha, Usense 106Ha na Kambuzi Halt 125Ha.
Skimu hizi zinafaa kwa shughuli za kilimo kwa kipindi cha mvua na kiangazi kwa kuwa zina maji ya kutosha. Pia. Ghala moja la mazao ya kilimo limejengwa katika kijiji cha Uruwira na ghala la Kambuzi Halt lipo katika hatua ya umaliziaji.
Hakuna mwekezaji mkubwa aliyejitokeza kuwekeza katika kilimo na ufugaji. Kuna fursa kubwa ya kuwekeza katika mitambo ya kukoboa mpunga, kusaga mahindi, kusindika nafaka za mafuta n.k.
Uzalishaji wa mazao katika Halmshauri ya wilaya ya Nsimbo kwa kipindi cha mwaka 20014/2015 na malengo kwa msimu 2015/2016 ni kama ifuatavyo:-
Mpanda to Tabora road
Anuani ya Posta: P.O.Box 688 Mpanda
Simu : 025 295 5164
Simu: 025 295 5164
Barua pepe: ded@nsimbodc.go.tz
Hatimiliki@2016GWF.Haki zote zimehifadhiwa